ABIRIA WANUSURIKA KWA AJALII YA GARI WILAYANI NGARA
Zaidi ya abiria 60 wamenusurika kupoteza maisha yao baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Dar es salaam kueleke Bujumbura nchini Burundi kuwaka moto wilayani Ngara Mkoani Kagera.
Tukio hilo limetokea leo Desemba 18 majira ya saa tano asubuhi katika eneo la Mkajagali kijiji cha Kumuyange, nje kidogo ya mji wa Ngara na kuhusisha basi la abiria la Kampuni ya Taqwa lenye namba za usajili T 964 BHS aina ya SCANIA.
Dreva wa gari hilo Bw John Peter amesema kuwa chanzo cha moto huo ni
hitilafu katika mfumo wa breki za magurudumu ya nyuma, yaliyotoa moshi
mkubwa na kuzalisha cheche zilizosababisha moto huo kutokea
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari hizi ambaye aliwahi kufika eneo
la tukio ni kwamba, mpaka majira ya saa tano na nusu asubuhi, moto huo
ulikuwa umedhibitiwa na hakuna abiria aliyepata madhara
Katika
jitihada za abiria na wafanyakazi wa gari hilo pamoja na watoa huduma
ya kwanza kutoka idara ya afya katika Hospitali ya Nyamiaga kuendelea kuzima moto huo baadhi ya mashuhuda wao walikazana kupora mali za abiria na kuzificha vichakani
Jeshi la polisi wilayani Ngara limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo limefanikiwa
kumtia mbaroni kijana mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja
aliyekuwa amebeba magunia madogo madogo ya bidhaa za wafanyabiashara
waliokuwa wakitokea dares Salaam kuelekea mjini Ngara na Bujumbura
nchini Burundi
Naye mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Constantine Kanyasu naye
alifanikiwa kuwasili eneo la tukio muda mfupi baada ya kutokea tukio
hilo na kuwasihi madereva kuwa makini na barabara za wilaya hiyo kwa
kuwa zina miteremko mikali na wapunguze mwendo kasi wakati wa safari zao
Aidha Kanyasu amedai kwamba wananchi
wanatakiwa kuimarisha uzalendo na kuwa na moyo wa huruma panapotokea
matukio kama hayo na kuacha tabia ya udokoza kwani kufanya hivyo
wanajiingiza kwenye matatizo ya kulitumikia gereza na kuathiri mfumo wa
maisha ya familia zao.
Na Shaaban Ndyamukama December 18, 2013