CHRISTIAN BELLA AOMBA KUSHIRIKI TAMSHA LA GURUMO JUMAMOSI HII TCC CLUB
MWIMBAJI anayesadikika kuwa na sauti tamu zaidi kwa sasa, Christian Bella kutoka Malaika Music Band, amesema atashiriki tamasha la Gurumo litakalofanyika Jumamosi hii kwenye viwanja wa TCC Club Chang’ombe.
Mratibu wa tamasha hilo, Juma Mbizo amesema Christian Bella, ameomba awekwe kwenye ratiba ya waburudishaji ambapo atapanda kuimba japo wimbo mmoja kama ishara ya kuonyesha kuukubali mchango wa gwiji Muhidin Maalim Gurumo.
Kama ilivyoelezwa hapo awali, tamasha la Gurumo, limeandaliwa mahsusi kwaajili ya kumuaga kwenye muziki wa jukwaani baada ya kutangaza rasmi kustaafu.
Mbizo ameongeza kuwa Christian Bella amesema miongoni mwa kazi anazozikubali sana hapa nyumbani, ni kazi za Msondo Ngoma chini ya Gurumo.