JAMBO BUKOBA YABORESHA SHULE ZA MSINGI WILAYANI NGARA
KAGERA Shirika lisilo la jambo Bukoba lililoko mkoani Kagera limetoa msaada wa kujenga baadhi ya miundombinu ya shule tano za msingi kwenye wilaya kadhaa mkoani humo kwa lengo la kukuza vipaji na taaluma kwa wanafunzi wa shule hizo.
Mratibu wa shirika hilo Bw Steven Gonzaga amezitaja shule shule hizo kuwa ni Rulenge (Ngara) matundu manne ya vyoo , Tumaini (Bukoba Manispaa) madarasa mawili na ofisi ya walimu, Kalalo (Karagwe) darasa moja na Kishoju (Muleba ) iliyotengenezewa madawati 60.
Amezitaja shule nyingine kuwa ni Kasambya (Misenyi) ukarabati wa madarasa mawili na ofisi ya walimu, Kiruruma (Biharamulo) ujenzi wa darasa moja na Karwoshe BK vijijini ukarabati wa madarasa mawili na ofisi ya mwalimu mkuu.
Kwa upande wake afisa elimu wilayani Ngara Simon Mumbee amesema kuwa licha ya jamii kuchangia miradi kwa kutumia rasilimali zao bado wanahitajika kushirikiana na serikali kupunguza changamoto za miundombinu ya kujifunzia
Mumbee amesema kuwa idara yake kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya hiyo inahamasisha kutenga fedha kwa ajiri ya maboresho ya mazingira ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za walimu na kuweka samani na vitabu vya kutosha
Hata
hivyo Afisa mipango wa halamshauri ya wilaya ya Biharamulo Zabron
Janga kwa niaba ya mkurugenzi wake Nassibu Mbagga amesema licha ya
kupata msaada huo jamii haina budi kuendelea kuchangia miundombinu
inayokosekana.
“Jamii
haina budi kuchangia miradi ya maendeleo katika kupunguza changamoto
za miundombinu katika taasisi za serikali ili kuweza kuboresha maisha ya
wananchi wanaohitaji taaluma ndani na nje ya nchi”. Alisema Janga
Aliongeza
kuwa jamii inategemea sana kupata misaada na kuzidi kuathiri watoto wao
katika kupata taaluma kwenye sekta ya elimu pamoja na miundombinu
mingine katika sekta ya afya Maji na barabarahuku ikichtumia gharama
kubwa kuchangia anasa kwenye sherehe na harusi mbalimbali.
Afisa Elimu Wilaya ya Ngara Ndg Simon Mumbee akikagua nembo ya Jambo Bukoba.
Pichani wanafunzi wa shule ya msingi Rulenge wilayani Ngara wakifurahia kujengewa vyoo kwa shilingi milioni 4 na jambo Bukoba ambapo jamii ya shule hiyo imechangia 38% ya ujenzi kwa kukusanya vifaa vinavyopatikana katika mazingira yao
Afisa Elimu Wilaya ya Ngara Ndg Simon Mumbee katikati katika picha na wa jumbe wa kamati ya shule ya msingi RulengeAfisa Elimu Wilaya ya Ngara Ndg Simon Mumbee akikagua nembo ya Jambo Bukoba.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Rulenge Ndg Mashaka Makemba akitoa taarifa ya ujenzi na nguvu ya jamii.
Steven Gonzaga katika hafla ya kukabidhi Choo cha wanafunzi
Steven Gonzaga mratibu wa Jambo Bukoba akikabidhi choo cha kisasa kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya Rulenge.
Habari/picha na Shaaban Ndyamukama Ngara