MICHUANO KUTAFUTA MISS WA WILAYA- NGARA
Pichani ni Wanyange wanaowania miss Ngara katika mitindo mbalimbali ya maonesho wakiwa katika mazoezi ya Pamoja
Na Shaaban Ndyamukama
Kufuatia kuwepo kwa sikukuu za chrismas na mwaka mpya watoto wa kike katika wilaya ya ngara wameanza kujitokeza kwa ajili ya shoo ya kumtafuta miss Ngara na kuinua vipaji mkoani kagera itakayofanyika Desemba 31 mwaka huu wilayani humo
Maandalizi ya kumtafuta miss Ngara mwaka huu wilayani humo yanaendeshwa na chini ya mhamasishaji wake Godwin Bucha (G2B) ambaye ni mwanaburudani katika kundi la Vijana chini ya ufadhili wa Paradise Hotel na Happy Fassion za mjini Ngara
Vijana wa kike wanaojiandaa kuwania nafasi hiyo ni saba kutoka maeneo ya mjini hapo ambao tayari wameanza kujitokeza kuwania taji hilo ni Marry Edward (19) Edina Charles (18) na Marry Julius (21) wengine wanaendelea nataratibu za usajiri na muda si mrefu wataonekana katika ukurasa wetu wa habari
Akiongea na Bukoba wadau G2B amesema vipaji vya vijana hasa maeneo ya pembezoni havitambuliki hivyo kuna haja ya kuwainua na waweze kujiamini katika shughuli zao za kuinua maisha.
Amesema kuwa mshindi wa kwanza katika michuano hiyo atajinyakulia Vifaa vya saloon ya kike wa pili atapata Jokofu na watatu zawadi yake ni cherehani “Malengo zaidi ni kuwajenga kuwa wajasiliamali kisha kukuza mitaji kwa kujikinga na vitendo vya kudhalilisha jinsia yao”.Alisema G2B
Amedai kuwa wanaopenda kuibua vipaji vya vijana wajitokeze na siku hiyo ya mchuano watakuwepo wadasu mbalimbali wa maisha ya vijana ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo Bw Costantine Kanyasu.