MKUU WA MKOA WA KAGERA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO NA KUHIMIZA UKAMILISHWAJI WA MIRADI YA MATOKEO MAKUBWA SASA
Mkuu wa Mkoa Kagera Akikagua Vyumba vya Maabara za Sayansi, Madarasa Nyumba ya Mwalimu Katika Wilaya ya Karagwe.
Mtoto Aiteka Maji na Kufurahia Mradi huo Katika Kijiji KibingoWilaya ya Kyerwa Mradi huo Umekamilka kwa Asilimia Mia moja.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Akihakikisha Kama Maji yanatoka Wilayani Kyerwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Akisikiliza Kero za Wananchi na Kutoa Ufumbuzi wake Katika Ziara ya Kuzunguka Mkoa Mzima. Aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Bi Darry Rwegasira.
Tanki la Maji Nyaishozi Wilayani Karagwe Ambapo Mradi umekamilika kwa Asilimia 75
Maji ni Uhai cheki watoto wanavyotabasamu
Mkoa wa Kagera umeanza kutekeleza mkakati wa serikali wa Matokeo Makubwa Sasa ili kuwaletea wananchi maendeleo ya haraka katika sekta za Kilimo, Maji, Elimu, Uchukuzi, Nishati na Madini, na Uwezeshaji wa wananchi kupitia mapato.
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe katika kuhakikisha mkoa wake
unatekeleza mkakati huo wa Matokeo Makubwa Sasa amefanya ziara ya mkoa mzima
ili kuhimiza, kukagua na kupokea miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya
mkakati wa Matokeo Makubwa Sasa.
Elimu,
katika sekta ya elimu Mhe. Massawe alikagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba
vitatu vya maabara za masomo ya sayansi
kila shule, aidha kupokea vyumba ambavyo tayari vimekamilika kwa kila
wilaya na kuhimiza ujenzi wa nyumba za walimu na kukamilisha
vyumba vya maabara.
Maji,
katika mkakati wa Matokeo Makubwa sasa serikali imejipanga kuhakikisha
inatekeleza miradi ya maji kwa vijiji kumi ambapo Mkuu wa Mkoa alikagua
maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo ya maji kwa wananchi na kujionea miradi
ambayo tayari imekamilika na kutoa huduma kwa wananchi.
Kilimo,
mkoa wa Kagera umejipanga kutokomeza ugonjwa wa mnyauko ambapo Mkuu wa Mkoa
ametangaza operesheni tokomeza Mnyauko katika mkoa wa Kagera kuanzia Januari
2014 .Zaidi ya asilimia 85 ya wananchi wa mkoa wa Kagera wanategemea zao la
ndizi kama zao kuu la chakula na biashara.
Nishati
na Madini, serikali kwasasa inatekeleza
mkakati wa kupeleka umeme vijijini ili wananchi waishio vijijini waweze kupata
umeme. Miradi mingi kwa hivi sasa inaendelea kutekelezwa ya kupeleka umeme
vijijini.
Katika
Wilaya ya Misenyi mradi wa umeme
unaotekelezwa hivi sasa ni wa kutoa umeme Bunazi Makao Makuu ya Wilaya kuelekea
Mtukula mpakani mwa Tanzania na nchi ya Uganda ambapo vijiji vyote ambavyo vipo
katika eneo hilo vitapatiwa umeme kufikia
Desemba 31, 2013.
Wahamiaji
Haramu, Mkuu wa mkoa wa Kagera kupitia kaulimbiu ya “Hakuna wa Kubaki na Hakuna
wa Kurudi” katika ziara yake ya mwisho wa mwaka 2013 amekuwa akiwahimiza
wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kamati za ulinzi na usalama za Wilaya
ili kuhakikisha wahamiaji haramu wote wanarudi kwao na hakuna kurudi.
Pia
Mhe. Massawe katika ziara yake alifanya mikutano ya hadhara na wananchi na kuwakumbusha kuendelea
kujikinga na ugonjwa wa UKIMWI ambao sasa unaonekana unaendelea kupanda tena
katika mkoa wa Kagera kutoka asilimia 3.4 hadi 3.7 Pia Mkuu wa Mkoa aliwaeleza
wananchi jinsi serikali inavyotekeleza mkakati wake wa Matokeo Makubwa Sasa.
Na Sylvester Raphael