Bukobawadau

MSICHANA MWINGINE WA KITANZANIA AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA

Nchi ya Tanzania imeingia tena kwenye headline kuhusiana na suala la Madawa ya kulevya baada ya kukamatwa tena kwa Mtanzania mwingine akisafirisha Madawa hayo toka Thailand kuelekea Macao nchini China jumanne iliyopita.
Mtanzania huyo ni msichana ana jumla ya umri wa miaka 28 aitwae Jackie Clief alikamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya Heroin huko Macao nchini China

Dawa hizo zimekutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na wana usalama kisha kufanyiwa X-ray ambapo baada ya kufanyiwa X-ray alikutwa na jumla ya vidonge 66 vikiwa na thamani ya dola za kimarekani 137,72.

Msichana huyu aliliambia Jeshi la Polisi nchini China kwamba alikua akisafiri kuelekea Guangzhou ambao ni mji ulio chini ya jimbo la Guangdong huko China,Inasemekana Msichana huyu amewahi kushiriki video mbalimbali ikiwa ni pamoja na video ya Nataka kulewa ya Diamond
Picha wakati wa mahojiano na wanahabari
Next Post Previous Post
Bukobawadau