MWIGULU AMLIPUA MBOWE BUNGENI NI KUHUSU KUTUMIA VIBAYA MADARAKA YAKE!!
Mh.
Mwigulu nchemba madelu, mbunge wa iramba magharibi katika mwongozo
alioomba kwa spika wa bunge asubuhi hii amemlipua kiongozi wa kambi ya
upinzani bungeni FREEMAN MBOWE kwamba ametumia madaraka yake vibaya na
kuharibu image na heshima ya bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania
kwa kukatisha ziara ya kikazi ya mbunge wa viti maalumu chadema mkoa wa
arusha joyce mukya ambaye alisafiri kwa kazi za kibunge kwenda Dominica
Republic,lakini akiwa new york, MUKYA alipokea simu ya MBOWE kuwa
akatize safari yake na kwenda Dubai aungane naye kwa "kazi maalumu' .
MWIGULU ameomba mwongozo kuwa uongozi wa bunge umchukulie hatua mh
mbowe kama mtu binafsi badala ya hivi sasa ambapo taasisi nzima ya bunge
inachorwa vibaya mbele za jamii ambapo Habari zilizopo kwenye top page
za magazeti ya leo yamelichafua bunge zima kumbe mhusika mkuu ni mbowe
ambaye ameelezwa kuwa alimwamuru joyce mukya arudi kutoka safarini
badala yake aende dubai kwa kazi maalumu wakati tayari alishapokea posho
ya bunge kwa safari ya kikazi.