Bukobawadau

RC KAGERA AHAMASISHA AMANI NA MSHIKAMANO ARFIKA MASHARIKI

Na Shaaban Ndyamukama December 21, 2013
NGARA
Mkuu wa mkoa wa Kagera kanali mstaafu Fabian Masawe amewataka wananchi mkoani humo kuimarisha  amani na mshikamano na nchi jirani katika kukuza jumuia ya Afrika ya Mashariki
Kanali Masawe amesema hayo leo December 21,2013 katika matembezi ya hisani ya kilomita 29 kutoka ngara mjini hadi mji mdogo wa Kabanga wilayani Ngara ya kuhamasisha amani  na usalama yaliyoandaliwa na Radio Kwizera kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wilayani humo
Amesema kuwa wilaya zote mkoani humo zinapakana na nchi nne za Afrika mashariki yaani Rwanda Burundi Uganda na sehemu ya Kenya katika ziwa viktoria hivyo wajibu wa wananchi ni kuimarisha mahusiano katika kulinda Amani ya jumuia hiyo
"Wananchi tumieni fursa zilizopo katika maeneo yenu kujiongezea  mapato  kama vivutio vya utalii na fursa ya ardhi na rasilimali nyinginezo ili  kujikwamua kiuchumi kwenda sanjari na nchi wanachama wa jumuia na mataifa mengine duniani".Alisema Kanali Masawe.
Hata hivyo mratibu wa matembezi ya hisani ya kuhamasisha usalama na Amani  Joyce Ngalawa amesema malengo ya mayembezi hayo nik kudumisha umoja na mahusiano ya taasisi na Mashirika mbalimbali yanayofanya kazi wilayani humo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau