SAMAHANI PICHA HIZI ZINATISHA:Apoteza maisha kwa kuchomwa mshale wenye sumu
Mtu mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja amekutwa amekufa jana katika uwanja wa posta ya zamani wilayani Ngara mkoani Kagera akiwa amechomwa mshale shingoni unaosadikiwa kuwa na sumu.
Mkuu wa jeshi la polisi wilayani Ngara Abeli Mtagwa amesema mtu huo ameonekana jana Desemba 11 saa 12 asubuhi baada ya wapita njia kumkuta jirani na uwanja huo na kwenda kutoa taarifa katika kituo chapolisi ngara mjini.
Amesema mwili wa mtu huyo umehifadhiwa katika hospitali ya Nyamiaga kwa ajili ya kuweza kutambuliwa na ndugu zake la jeshi hilo linafanya uchunguzi kuweza kubaini watu waliohusika na mauaji ya mtu huyo.
Hata hivyo baadhi ya wananchi walikuwa katika eneo la tukio wamesema huenda mtu huyo alikuwa katika harakati za wizi na kuchomwa mshale na katika kukimbia ndipo sumu ilimzidia na hatimaye kufariki akiwa amefika kwenye uwanja huo
Kwa hisani ya NGARA Na Shaaban Ndyamukama