Skylight Band yaporomosha burudani ya kukata na shoka X-MASS ndani ya kiota cha Escape One
Vijana wa Skylight Band wakionyesha manjonjo yao kwa mashabiki wa Band hiyo wakati wa sherehe za X-MASS ndani ya fukwe za kiota cha Escape One walipotoa burudani ya kukata na shoka kwa mashabiki wao.
Aneth Kushaba AK47 akifanya yake jukwaani huku akipewa back up na Joniko Flower, Winnie pamoja na Digna Mbepera.
Mary Lukos akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band katika kusheherekea sikukuu ya X-MASS ndani ya kiota cha Escape One.
Mashabiki wa Skylight Band mdogo mdogo wakijisogeza kwa dancing floor.
Joniko Flower akiwasogeza mashabiki kwa dancing floor kuwarusha na gwaride la aina yake.
Mguu wa kushoto mbele wa kulia nyuma....Ya chuma chuma nataka mukanda Ya chuma chuma.....!!! Hapo ni gwaride mwanzo mwisho...
Mheshimiwa Bernard Bundala na mdau Emmanuel Francis wakionyesha umahiri wao katika kusakata sebene la Skylight Band kwenye sherehe za X-MASS.
Hapo sasa twende kazi...!!
Mdau Emmanuel Francis akifanya yake, njoo leo Thai Village akifundishe style hii mpya ya Skylight Band.
Mashabiki wa Skylight Band wakisebeneka na burudani ya kukata na shoka.
Rapa wa Skylight Band Sony Masamba akimpagawisha shabiki wake.
Palinogaje wewe uliyekosa tunakupa pole tukutane leo pale Thai Village ufurahie Holiday yako na Skylight Band.
Mpiga Solo wa Skylight Band Allen Kisso a.k.a Mundende akimchizisha shabiki na upigaji wake Gitaa.
Mrs. Kisso akisebeneka na wifi yake Digna Mbepera.
Kwa raha zao kwenye upepo mwanana wa Baharini ndani ya fukwe za kiota cha Escape One, Mikocheni jijini Dar.
Daudi Tumba akifanya yake jukwaani, ni kiungo muhimu sana kwenye Live Band.
Lubea wa Skylight Band akishow love na Super Model Neema Mbuya na mdau kwenye kiota cga Escape One.
Mdau Alois Ngonyani akishow love na mashemeji zake.
Mdau Fredy Tony akishow love......!!!
Wadau wa Skylight Band kutoka Kijitonyama nao walijumuika na Band hiyo kusheherekea X-MASS ndani ya fukwe za kiota cha Escape One jijini Dar.
Fans wa Skylight Band.
Mdau William Malecela a.k.a LEMUTUZ akishow love na Mbabes mkareeeee ndani ya kiota cha Escape One.
Mdau nambari moja wa Skylight Band Alois Ngonyani akishow love na Sam Mapenzi wakisherekea sikukuu ya X-MASS Escape One jijini Dar.
Wadau Batani na Skylight Band ndani ya kiota cha Escape One kilichopo Mikocheni jijini Dar.
Aneth Kushaba AK47 akishow love na shabiki wake.
Watu wa ukweli kwenye muziki wa wastaarabu.....!!
Wenye mbeleko haya wenye vibwaya mulele twende kazi.....!!!
Mduara ulihusika pia....!!
Shazi la kumwaga usiipimie Skylight Band....!!! tukutane leo jioni Thai Village Masaki tufurahi pamoja.
Winnie wa Skylight Band akipata Ukodak na wifi yake Mrs. Kisso.