Bukobawadau

WAKULIMA wadogo wanakabiliwa na ukosefu wa soko la mazao ya biashara na chaku inShar

WAKULIMA wadogo wanakabiliwa na ukosefu wa soko la mazao ya biashara na chakula.
Wakulima hao walitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti katika kongamano la wakulima kuibua changamoto za kilimo lililoandaliwa na mtandao wa vikundi vya wakulima wadogo Tanzania (Mviwata), mkoa wa Kagera.
Dominic Mwombeki, mkulima wa miwa kutoka wilayani Missenyi, alisema gharama za uzalishaji ni kubwa ikiwemo matumizi ya dawa za mimea.
Mwombeki alisema kutopata pembejeo za kustawisha miwa safi ni moja ya vikwazo katika shughuli zake na kusema Kiwanda cha Sukari cha Kagera hakikidhi mahitaji ya kipato cha wakulima wa miwa.
Alisema wakulima hawana mamlaka ya kupanga bei ya mazao yake; anapangiwa na wanunuzi huku akitoa mfano wa kahawa.
Kwa mujibu wa mkulima huyo lipo tatizo la kuwekewa mipaka ya kuuza mazao yao wakati wanalima ili kuondokana na umaskini lakini wanakabiliwa na mipaka ya soko.
Julius Rwakyendera ambaye ni mkulima wa kahawa katika kijiji cha Gwansel, wilayani Muleba, alisema tatizo lao ni mabadiliko ya tabianchi yaliyosababisha ndizi za asili kupotea.
Rwakyendera, alisema ndizi za kisasa haziliki bila mboga, tofauti na ndizi za asili ambazo huliwa zenyewe.
Alisema waliamua kujiunga na Mviwata ili kuwa na sauti moja itakayofikisha kilio chao serikalini.
Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya Mviwata  taifa Projestus, alisema malengo ya mtandao huo ni wakulima wadogo wote kujiunga.
Next Post Previous Post
Bukobawadau