WANANCHI NGARA WAITISHIA HALMASHAURI YAO KWA KUGAWA ARDHI BILA KUWASHIRIKISHA
Pichani ni mahudhurio ya wananchi katika mkutano wa hadhara
Na Shaaban ndyamukama December 18,2013
NGARA: SERIKALI ya kijiji cha Kasulo wilayani Ngara mkoani Kagera imemkataa mwekezaji aliyepewa ardhi ekari 50 na halmashauri ya wilaya yao kwa madai kuwa wananchi hawakushirikishwa wakati anaoneshwa ardhi na kuimiliki
Mwenyekiti wa kijiji cha kasulo Bw. Yusuph Katura amtoa kauli hiyo jana kwenye mkutano wa hadhara wa wananchi wake pamoja na watu walio na mashamba katika msitu wa Lumasi uliofanyika katika kitongoji cha Benaco wilayani humo
Bw. Katura amesema kuwa uongozi wa kijiji na kata haukushirikishwa wakati mwekezaji ambaye ni kanisa la ELCT KKKT katika kutoa eneo hilo ambapo alitakiwa kupaendelezwana kamati ya maendeleo ya kijiji na kuridhiwa na mkutano mkuu
Alisema wanaogawa eneo hilo kutoka Halmashauri wamefika wilayani hapo baada ya wakimbizi kuondoka waliokuwa katika ardhi hiyo na wananchi ndio walishiriki kupanda miti ambapo mpaka sasa ni miaka 3 tangu apatiwe eneo hilo
“Kwa ridhaa ya wananchi walio nichagua mwekezaji aondoke mara moja vinginevyo mkurugenzi ataona maamuzi ya wananchi hapo baadaye”Alisema
Alidai kuwa uoungozi wa kata ya kasulo unashikilia msimamo wake kuwa na kwamba msitu wa Lumasi na ardhi ya eneo hilo ni mali ya kijiji cha kasulo na kukataa kuwa halmashauri ya wilaya haina ardhi wala msitu katika eneo hilo
Mkutano ulioitishwa na mkuu wa wilaya ya Ngara Costantine Kanyasu lakini kutokana na majukumu ya kiutendaji katibu tarafa ya Nyamiaga Bw. Godian Bagombweki ndiye alimwakilisha ambapo diwani wa kata ya Kasulo Bw. Phillibart Kiiza amedai kuwa msimamo wa kata ni kwamba ardhi ni mali ya serikali ya kijiji
Bw. Kiiza amesema kuwa uongozi wa kata pamoja na serikali ya kijiji cha kasulo wanapinga tamko la halmashauri ya wilaya lililotolewa na afisa mistu wa wilaya Ngara Bw. Philipo Ileta kuwa halmashauri itaendelea kuvuna miti kwa miaka mitatu ijayo na kwamba hawatakubali suara hilo
“Naungana na wanachi wa kijiji cha Kasulo kwamba wakati mwekezaji huyo anapata eneo hilo watendaji wa idara ya ardhi na misitu walifanya kinyume cha sheria ya ardhi namba 4 na 5 ya mwaka 1999”.Alisema diwani huyo
Kwa upande wake mwakilishi wa mkuu wa wilaya ambaye alikuwa katibu tarafa ya Nyamiaga Bw. Godian Bagambweki amesema kuwa uongozi wa halmashauri unapaswa kutafakari maoni ya wananchi na kufanya makubaliano ili kumaliza mgogoro kabla ya kutokea kwa athari za uvunjifu wa Amani.