BODI YA BARABARA YA MKOA WA KAGERA YAZINDUA DARAJA LA MTO KANONI MANISPAA YA BUKOBA
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Fabian Massawe akikata utepe katika uzinduzi wa Daraja la Mto Kanoni.
Mkuu wa mkoa wa KAGERA, Kanali mstaafu Fabian Massawe akipunga mkono mara baada ya kukata UTEPE
Mkuu wa mkoa wa KAGERA, Kanali mstaafu Fabian Massawe akipunga mkono mara baada ya kukata UTEPE
Kikao cha
Bodi ya Barabara cha Mkoa kimefanyika mkoani Kagera na kufanya tathimini ya
utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya barabara
katika ngazi za Halmashauri na Mkoa na kujadili changamoto mbalimbali
zinazoukabili mkoa katika kujenga, kutunza na kutumia barabara hizo.
Mkoa
wa Kagera unaokadiliwa kuwa na mtandao wa barabara zenye urefu wa kilomita
7,569.24 ambapo kati ya hizo kilomita
1,914.5 zinasimamiwa na Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa barabara (TANROADS)
Mkoa na Kilomita 5,654.74 zinasimamiwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Hali ya Barabara, Kwa mwaka 2013 idadi ya barabara
zenye urefu wa kilomita 1,745.26 sawa na asilimia 91 zilikuwa katika hali
nzuri, kilomita 166.24 sawa na asilimia 8.7 zilikuwa katika hali ya wastani na
kilomita 3 sawa na asilimia 0.3 zilikuwa katika hali mbaya.
Katika
Bajeti ya mwaka huu (2013/14) fedha za barabara kwa Mkoa wa Kagera jumla ya shilingi
bilioni 14.89 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 9.019 zimetolewa kwa Meneja wa
TANROADS Mkoa na shilingi bilioni 5.871 zimetolewa kwa Wakurugenzi wa Mamlaka
za Serikali za Mitaa.
Kikao
hicho kiliweza kujadili utekelezaji wa fedha zilizoletwa mkoani kwa ajili ya
matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2012/13 pia na mwaka 2013/2014 ili
kuweka mikakati ya kuboresha utekelezaji
wa miradi ya barabara.
Katika
hatua nyingine wajumbe wa kikao cha Bodi
ya Barabara ya Mkoa wa Kagera wakiongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Mkoa wa
Kagera walifanya uzindizi wa daraja la mto Kanoni liloko katika Manispaa ya
Bukoba.
Katika
uzinduzi huo uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian I.
Massawe aliwasisitiza wananchi kulitunza daraja hilo bila kufanya uharibifu wa
kungoa vyuma vya pembezoni na kuvifanya vyuma chakavu.
Aidha
Mkuu wa Mkoa alitoa wito kwa Madiwani wa Bukoba ambao wanaendelea kugomea vikao
halali vya Baraza kukubaliana na kukaa ili kupitisha maamuzi ya kuwaletea
wananchi wa Maniaspaa ya Bukoba Maendeleo.
Kaimu
Meneja wa Wakala wa Mkoa wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Kagera Bw. Nazir
Kakindo akisoma taarifa ya ujenzi wa
daraja hilo lilokamilika kwa asilimia 90 alisema likikamilika ujenzi wake
utagharimu kiasi cha shilingi milioni 339,449,027 gharama hizo ni pamoja na
kuweka njia ya watembea kwa miguu katika daraja la Buyekera
Bw.
Kakindo alisema Mkandarasi anayejenga daraja la Kanoni ni Mulima Construction
Company ambaye anamalizia kazi ndogo ndogo zilizobakia wakati daraja hilo
likiendelea kutumika baada ya kukamilika kwa asilimia 90 na kuzinduliwa leo
tarehe 16/01/2014 na kuruhusiwa kuanza kutumika.
Daraja
la Kanoni lilikuwa limefungwa Takribani kwa miezi mitatu kuanzia mwezi Oktoba
2013
Na
Sylvestera Raphael
Afisa Habari Kagera