JAMBO BUKOBA YAWAJENGEA UWEZO WATOTO WA KIKE KUJIAMINI NA KUSHIRIKIANA NA WENZAO KATIKA ELIMU PAMOJA NA MICHEZO
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe Akiwahutubia
Wananfunzi na Wageni Waalikwa kwenye Ufunguzi wa Binanza la Jambo Bukoba
Kaitaba
Watoto Wakinyesha Michezo ya Kitamaduni na Mwalimu Wao
Baadhi ya Wanafunzi Waliohudhuria Bonanza Hilo
Clemence Mulokozi Kulia Aliyeweka Vidole Juu Mwanzilishi wa Jambo Bukoba na Mratibu wa Shirika Hilo Mkoani Kagera Bw. Gonzaga.
KAKAU BAND wakifanya mambo yao uwanjani
Mzungu Naye Hakuba ki Nyuma
Bw. Clemence Mulokozi Akifurahi na Kucheza na Watoto
Jambo Bukoba ni Shirika lisilokuwa la Serikali linalofanya kazi mkoani Kagera kwa kushirikiana na serikali ya mkoa. Mwanzilishi wa Jambo Bukoba anaitwa Bw. Clemence Mlokozi ambaye asili yake ni mkoani Kagera katika Wilaya ya Missenyi Kijiji Ishozi na anaishi nchini Ujerumani.
Watoto Wakinyesha Michezo ya Kitamaduni na Mwalimu Wao
Baadhi ya Wanafunzi Waliohudhuria Bonanza Hilo
Clemence Mulokozi Kulia Aliyeweka Vidole Juu Mwanzilishi wa Jambo Bukoba na Mratibu wa Shirika Hilo Mkoani Kagera Bw. Gonzaga.
KAKAU BAND wakifanya mambo yao uwanjani
Mzungu Naye Hakuba ki Nyuma
Bw. Clemence Mulokozi Akifurahi na Kucheza na Watoto
Jambo Bukoba ni Shirika lisilokuwa la Serikali linalofanya kazi mkoani Kagera kwa kushirikiana na serikali ya mkoa. Mwanzilishi wa Jambo Bukoba anaitwa Bw. Clemence Mlokozi ambaye asili yake ni mkoani Kagera katika Wilaya ya Missenyi Kijiji Ishozi na anaishi nchini Ujerumani.
Jambo Bukoba ilianzishwa mkoani
Kagera kwa kusaidia watoto hasa wanafunzi wa shule za msingi kuanzia miaka 5
hadi 19 kujenga afya zao kimichezo ili kujikinga na maabukizi ya UKIMWI, kuweka
haki sawa katika elimu kupitia michezo kwa wasichana na wavulana.
Shirika hili chini ya mwanzilishi
wake Bw. Mulokozi tangu kuanzishwa kwake mkoani Kagera limekuwa likiwafunza watoto katika shule za msingi kila wilaya michezo midogo midogo ya kujenga
ushirikiano wa pamoja hasa watoto wa kike kujiamini na kushirikiana zaidi na wenzao wa kiume.
Jambo Bukoba katika kuhakikisha
inapunguza unyanyapaa wa kuwatenga watoto wa kike katika jamii imeweza kueneza
elimu kupitia michezo kwa watoto wote kushirikiana kwa pamoja bila kujali
jinsia za watoto iwe katika masomo , michezo au katika shughuli nyingine za
kijamii.
Ili kuleta umoja katika mkoa kwa
watoto wa kiume na kike Jambo Bukoba kuanzia mwaka 2012 ilianzisha bonanza la
michezo kila mwisho wa mwaka la kuwaunganisha watoto kutoka shule mbalimbali
mkoani Kagera ili waweze kushirikiana pamoja kimichezo na kujenga kujiamini kwa
pamoja.
Bonanza la michezo la Jambo
Bukoba mwaka 2013 limefanyika mwaka huu 31 Januari, 2014 na kushirikisha Wilaya
zote za mkoa wa Kagera pamoja na
mwanzilishi wa Jambo Bukoba akiambatana na wenzake kutoka nchini Ujerumani.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Massawe alikuwa mgeni rasmi
ambapo katika hotuba yake ya ufunguzi aliwashukuru Jambo Bukoba kuanziasha
bonanza la michezo ili kuwajenga watoto kiakili na kujiamini aidha aliwahimiza wazazi kuwaruhusu watoto wao kucheza kwani michezo
nayo ni ajira.
Jambo Bukoba hutoa vifaa vya
michezo kama vile fulana na bukta za michezo, viatu na mipira katika shule mbalimbali mkoani Kagera. Vilevile
ili kuhakikisha watoto wanaendelea kupata elimu nzuri Jambo Bukoba imeanza
kukarabati miundombinu mbalimbali ya baadhi ya shule za msingi mkoani hapa.
Miundombinu hiyo ni pamoja na
madrasa ambayo yameharibika na kuhitaji ukarabati, kujenga matundu ya vyoo
mapya pamoja na kukarabati ofisi za walimu ambazo ziko katika hali mbaya ili
kuwarahisishia walimu kutekeleza majukumu yao vizuri ya ufundishaji.
Bw. Mulokozi anasema lengo lake
kubwa kuanzisha Bukoba ni kupunguza kasi ya watoto wa kike kuanzisha mahusiano
ya kimapenzi wakiwa wadogo, pia kupunguza unyanyapaa wa wtoto wa kiume kwa
wasichana ambapo Jambo Bukoba imepunguza tatizo hilo kwa kiasi kikubwa mkoani
Kagera.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2014