KOMANDO HAMZA KALALA USO KWA USO NA KAMANDA RAS MAKUNJA
Pichani Kamanda Ras Makunja na Komando Hamza Kalala
Juzi Kati ndani ya studio za Sibuka FM,Katika kipindi cha Pepeta Afrika,
mgeni rasmi nyota wa wiki alikuwa kamanda Ras Makunja kiongozi wa bendi maarufu barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU Ughaibuni,aka
Anunnaki Alien au "Watoto wa Mbwa". Kamanda Ras Makunja alifanya
maohijiano ya TV na Redio Sibuka, na alizungumuzia zaidi nafasi ya
muziki wa dansi wa Tanzania katika masoko ya kimataifa,
Mwanamuziki huyo wa Tanzania mwenye makao yake nchini Ujerumani
alitoa wito kwa watanzania waishio ndani na nje ya Tanzania
kuzipa nafasi bendi za muziki za Tanzania ili ziweze kuvusha muziki wake
nje ya mipaka ya Tanzania ,pia kufanya tour za kimataifa.
Ras Makunja aliutaja muziki wa dansi wa Tanzania "Bongo Dansi" kuwa una nafasi kubwa katika soko la kimataifa hiwapo Watanzania wenyewe watakuwa mstari wa mbele katika kuutanga na kuzipendekeza bendi za
Tanzania kwa maporomota na waandaaji wa maonyesho ya kimataifa.
Katika studio za Sibuka FM,jijini Dar-es-salaam Ras Makunja aliongozwa na mwanamuziki mkongwe nchini Komandoo Hamza Kalala ambaye aliutaja muziki wa
Ngoma Africa band aka FFU ughaibuni kuwa ni muziki ulipangiliwa kwa
mtindo wa kushambulia na kuteka washabiki katika masoko.
Komando Hamza Kalala alimtaja Kamanda Ras Makunja kuwa ni mojawapo wa wanamuziki wachache wa kitanzania wanao ipeperusha
bendera ya Bongo kimataifa bila ya uwoga.