RAIS KIKWETE ATANGAZA JUMATATU JANUARY 13,2014 SIKU YA MAPUMZIKO
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13,
2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote
kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini
Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea
miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.
Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa
Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa
madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika
historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.
Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar
yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi mitatu
baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.
Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa
Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati
alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika
kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametangaza kuwa kesho, Jumatatu, Januari 13,
2014, itakuwa ni Siku ya Mapumziko (Public Holiday) kwa Watanzania wote
kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais Kikwete ameutangaza uamuzi huo mjini
Zanzibar ambako leo ameungana na Watanzania na Wazanzibari wote kusheherekea
miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, mwaka 1964.
Mapinduzi hayo yaliyoongozwa na mwasisi wa
Zanzibar na Taifa la Tanzania, Hayati Abeid Amaan Karume yalifanikiwa kuung’oa
madarakani utawala dhalimu wa Sultan na kuwawezesha kwa mara ya kwanza katika
historia Waafrika walio wengine kujitawala ndani ya nchi yao wenyewe.
Yalikuwa ni Mapinduzi ya Zanzibar
yaliyofungua njia ya kuzaliwa kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar – miezi
mitatu baada ya Mapinduzi hayo – Aprili 26, 1964.
Naye Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Ali Mohamed Shein ametangaza kuwa kesho itakuwa
Siku ya Mapumziko Tanzania Visiwani kusheherekea miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Rais Shein alitangaza mapumziko hayo wakati
alipohutubia wananchi kwenye Uwanja wa Michezo wa Amaan mjini Zanzibar katika
kusherehekea miaka 50 ya Mapinduzi.
Mwisho.
Imetolewa na;
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS
Ikulu,
es
Salaam.
12
January, 2014