SALAAM ZA HERI YA MWAKA MPYA ZIKIENDELEA JAN 13,2014
Ndugu Murshid Hassan Byeyombo
Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji
wa Maruk Vanilla Farming and Processing Ltd
Ndugu Wadau,
Kwa niaba ya Wakurugenzi wa Maruk
Vanilla Farming and Processing (MVFP) Ltd nawatakia mwaka mpya wenye heri na
mafanikio katika mipango yenu. Sisi kama MVFP Ltd tunawaahidi kuendeleza
gurudumu la ukombozi wa Mkulima wa Vanilla na mazao mengine ya Biashara hasa
viungo (spices).
Mwishoni mwa mwaka jana
tulianzisha mpango maalumu wa kuongeza uzalishaji wa zao la vanilla kwa kugawa
marando (vines) mapya. Pia tuliweza kuanza ushamirishaji wa mazao mbadala ya
Biashara mkoani mwetu. Tumeweza kugawa zaidi ya miche 7500 ya vanilla na miche
800 ya pilipilimanga (black pepper) yote kwa wakulima wapya. Mpango huu
umeonyesha kuitikiwa vema na wakulima hivyo mwaka 2014 tutazidisha jitihada.
Mwaka huu tayari tumezindua
huduma ya MALIPO YA AWALI KWA WAKULIMA
WENYE DHARURA. Huduma hii ni maalumu kuwakwamua wakulima wa vanilla kifedha
wakati wakisubiri mavuno na mauzo ya mazao yao. Dharura zitakazo hudumiwa ni
zile zinazohusiana na Elimu na Afya kwa wanafamilia wa mkulima wa vanilla.
Tunatarajia kupanua mkondo mmoja wa huduma hii kufikia kuwa huduma kamili ya
Bima ya Afya kwa Wakulima.
Kama ilivyo ada, msimu wa mwaka
huu 2014 MVFP Ltd itaendeleza sera yake ya manunuzi ya vanilla kwa mkulima
ambayo wakulima hulipwa papo kwa papo pesa taslimu mara tu wanapofikisha mazao
yao kwenye kituo cha manunuzi. Tunaheshimu utaratibu huu kwani tunatambua kuwa
mkulima anauza mazao yake ili kujikomboa na kukidhi mahitaji mbalimbali. Kwa
kuwa mahitaji na shida zake hazisubiri baadae, hivyo malipo kufanyika muda
kitambo baada ya mauzo ni kumfanya mkulima ashindwe kutimiza haja zake. Na
hatma yake wakulima huacha kuhudumia mashamba, hung’oa miche na kulichukia
zao.
Kuna kila dalili kwamba bei ya
mapodo itapanda na hivyo kumfanya mkulima apate malipo mazuri. MVFP Ltd
tunazidi kuwasisitiza wakulima kuongeza uzalishaji na kujali miche yao. Pia
tunaishauri serikali na wadau wa maendeleo kumulika zao hili la vanilla. Tuna imani
kwamba vanilla ina uwezo mkubwa wa kubadili maisha ya wakulima iwapo itapata
msukumo stahili kutoka kwa wafanya maamuzi na watendaji wa vyombo vya
umma.
Mwisho tunapenda kuwashukuru na
kuwapongeza wamiliki na waendeshaji wa http://bukobawadau.blogspot.com/
kwa kazi nzuri wanayoifanya kuuhabarisha umma juu ya nini kinaendelea nyumbani
na duniani. Blog hii imetusaidia kwa njia ya “trickle-down effect”
ambapo wale walioko mbali na nyumbani, baada ya kusoma habari zetu hapa,
huamasisha walioko nyumbani kujiunga na kilimo cha vanilla. Tunaomba wadau
muendelee na moyo huu kwa maendeleo ya watu wetu na Kagera yetu.
Omutwale Innocent Mushaijaki
kutoka Ishozi Rutala lakini kwa sasa naishi jijini Dar es salaam na
kufanya kazi katika kampuni ya SCANAD kama media monitoring meneger,nawatakia heri na fanaka katika mwaka huu mpya wa 2014 na pia nasema
kwamba TWETOHYE TULEKELE OLWANGO , OKUTENDELANA N'ENOBI.
Mpindi Nshubuga;Nawapenda sana wana bukoba wote,Ujumbe ni kwamba umoja ni nguvu utengano ni udhaifu tudumishe undugu na tuzidi kujuana kwenye shida na raha.
Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kufika mwaka 2014 Nawatakia mema wadau wote ktk mwaka huu.Letty
Naitwa Julius Lubega;Mwaka huu hatuhitaji kumtafta mchawi, Nawatakieni 2014 wa tukijua kudharau ni chanzo cha umasikini. Peace to you bukobawadau blogsport God bless.
Hodi hodi, naitwa Lilian napenda kuwatakia wana bukoba wote pamoja na ndugu jamaa na marafiki heri ya mwaka mpya, Mungu awajalie baraka tele. May we experience lot of it in this 2014 also i thank bukobawadau blog for your effort, guys hav done a good thing kufungua hii blog kweli tunaona mambo mengi yanayoendelea bukoba hadi raha. shukrani sana and all the best in 2014.. God bless
Salma Komba (mama frank) Nawatakia heri ya mwaka mpya wa Tanzania wote popote walipo ujumbe tudumishe amani tulionayo

Finally 2013 Came To An End.
Happy New Year For All Of U.As the Year Goes on,
You are also get old
Before leaving let me Wish you All for You Good Future and full of
success as the last year was very challenging but still we belive we can
still make it with our life goals as i belive where theirs a will
theirs a way,so just axcept the challanges and make sure your playing a
right game to achive the success.And also thanks alot mc for updating
us withl all the news around the world ,bukoba we are one.Rehena Gulam.
Salma Mkalibala kutoka mtwara, Ujumbe nawatakia watanzania Wenzangu heri ya Mwaka wa mafanikio
Siraji Majura kutoka Kemondo;Ujumbe Maisha yakikupiga chenga Ruksa kucheza Rafu!
Annah Kyungay; “Anyone who has never made a mistake has never tried anything new” 2014 Jipange.