Bukobawadau

TASWIRA MAANDALIZI YA KIPINDI KUHUSU MAREHEMU JUSTIN KALIKAWE:BY MUBELWA BANDIO

 Mdau Mubelwa Bandio kupitia ukurasa wake wa facebook ameweza kueleza kwamba,moja mipango aliyokuwa nayo ni  kutengeneza kipindi juu ya Justin Kalikawe.
Na sasa anamshukuru Mungu kuwa amefanikisha sehemu ya mpango huo ambapo kwa siku ya Jana amepata muda mfupi kuhojiana na mjane wa Marehemu Kalikawe Bi Georgia Kalikawe pamoja na binti yake mkubwa Abayo pia ndugu wa familia ya Kalikawe ambao Wameeleza mikakati waliyonayo juu ya kazi za Marehemu Justin Kalikawe 
Bukobawadau Blog tunakupatia fursa ya mtiririko wa mahojiano hayo ,Mengine mengi yanafuata kipindi kikikamilika.

 Kipindi hiki kinaandaliwa na  Mwanahabari wa Jamii Production kutoka nchini Columbia, Maryland , Mdau Mubelwa Bandio  pichani kulia akiwa katika mahojiano na Ras Nold ambaye ni Mtoto wa Kaka wa Hayati Justin Kalikawe hakika ameweza kunena mengi mema kuhusu Marehemu Justin Kalikawe.
Mahojiano na Mjane wa Marehemu Justin Kalikawe Bi Georgia Kalikawe
Mahojiano na Abayo Binti mkubwa wa Justin Kalikawe
Mdau Bandio katika Kaburi la Marehemu Justin Kalikawe.
Maandalizi ya kipindi hiki bado yanaendelea, hapa ni wakati wa mahojiano na mmoja wa Marasta nao wanamengi ya kusema kuhusu Marehemu Kalikawe.
 Mahojiano na Mdau Burhan Bushako, maarufu kama Ras Bitto,Yeye ni Mpwa wa Hayati Justin Kalikawe ameweza kuelezea mengi  kuhusu  Marehemu mjomba wake!
 Mwanahabari mahiri wa Jamii Production Mdau Mubelwa Bandio katika picha na Mpwa wa Marehemu Justin Kalikawe Ndg Burhan Bushako.
Mubelwa na Watoto wa ndugu zake Justin Kalikawe ,kulia aliyeachia Rasta ni Burhan Bushako. Mtoto wa dada yake Justin  Kalikawe na katikati  ni Ras Nold,Mtoto wa Kaka wa Justin,Marehemu Mzee David Kalikawe.
Ras Nold Kalikawe.
 Mdau Mubelwa Bandio katika picha ya pamoja na Mjane wa Justin Kalikawe Bi Georgia na binti yao mkubwa Abayo (katikati) baada ya mahojiano yaliofanyikanyumbani kwao Kitendaguro Bukoba.

 CREDIT; Mubelwa Bandio,shukrani kubwa kwake Mdau Nicolas Ngaiza wa  88.5Kasibante Fm


Next Post Previous Post
Bukobawadau