Bukobawadau

TASWIRA SIKU MOJA KABLA YA TAARIFA YA CAG MJINI BUKOBA JAN 16,2014.

 Ndani ya Viunga vya Manispaa ya Mji wa Bukoba, Jioni ya leo Alhamisi 16,2014 Camera yetu inakutana na wadau mbalimbali wakijadili kitendawili cha nani atawajibishwa kufuatia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) , Ripoti hii inatolewa siku ya Kesho Ijumaa Jan,17,2014
Yupo Mdau Abdumalick Tibabimale kama anavyo onekana akiteta jambo na mwenzake
Kijiwe cha Seneti ambacho ni  'Tanuru la Siasa' mjini hapa tunakutana na Mzee Maulid Kambuga naye yupo katika hali ya Sintofahamu kufuatia hali hii iliyozua mtafaruku CCM Bukoba.
Miradi iliyokuwa inalalamikiwa ni upimaji wa viwanja 5,000 unaodaiwa mkopo wake wa sh bilioni 2.9 kutoka Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji (UTT) haukufuata taratibu, na wananchi hawakushirikishwa ipasavyo.Upo pia ujenzi wa soko ambapo meya anadaiwa kusitisha malipo ya ushuru na kutaka kuwaondoa wafanyabiashara bila kufuata utaratibu.Camera yetu ikiwa bado maeneo haya ya Seneti ,nje ya Soko Kuu Mjini Hapa, inakutana na Mama mpambanaji 'Mama Stella'akiwa nje ya ofisi yake akiendelea na majukumu.
Mdau Jumanne Bingwa.
Kikubwa ni homa ya matokeo ya mjadala wa ripoti ya CAG.
Macho na matukio ya Watu wote mjini hapa ni juu ya Ripoti ya CAG
Mpaka tunaingia Mtamboni jioni hii tayari tayari Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe. Agrey Mwanri yupo mjini hapa kutoa majibu ya ripoti ya CAG itakayojidhihirisha hapo kesho

NOTE;KUPATA MATUKIO YA JANA AU YA MUDA MCHACHE ULIOPITA TUNAKUKUMBUSHA KUPITIA 'OLDER POST'KILA MWISHO WA UKURASA WETU, KUPATA UPDATE KUPITIA EMAIL YAKO JIUNGE NASI KWA KUWA FELLOW/MEMBER KWA KUJOIN NASI  PEMBENI KULIA MWA BLOG YETU.


Next Post Previous Post
Bukobawadau