TRUST IS NOT GIVEN OR RIGHT.TRUST IS EARNED
Usikae kilasiku kumlalamikia
mpenzi wako eti “mbona huniamini?” “sikuhizi umepunguza kuniamini”
“utasemaje unanipenda kama huniamini?”
‘minaona hapa hatuaminiani!”
Na maneno mengine tele kisa tu umehisi huaminiwi. Jiulize kuto
kuaminiwa kumeanza lini? Nini kimesababisha? Kumbuka sio haki yako
kuaminiwa, na wala kuaminiwa hakulazimishwi ila mazingira ndiyo
yanamlazimisha mtu kumuamini mwingine. Kamwe usitegemee kuaminiwa
wakati mazingira unayojenga ni ya kuiua imani juu yako. Kabla haujaanza
kulalamika kuwa huaminiwi jenga au rekebisha mazingira ya kuaminiwa
kwanza. Na kama mazingira unayoyaweka ni yakutokuaminika basi usimlaumu
mtu mwingine kwa kutokukuamini, jilaumu wewe mwenyewe. Usijidanganye
hata siku moja kuwa kuaminiwa hushuka tu ‘automatically’ NEVER,
Kuaminiwa kunaandaliwa na kujengewa mazingira.