Bukobawadau

UFAFANUZI WA EZEKIEL MAIGE(MB) JUU YA YALIYOJIRI KWENYE MEDANI ZA SIASA -STAR TV

Wapendwa,

Salaam za pilika za maisha?

Nimeona ni vema nikawafafanulia, kwa baadhi ambao hamkufuatilia kipindi cha Medani za Siasa kilichorushwa na Star TV jana mchana.
Nimeona nifanye hivyo baada ya upotoshaji wa kitoto, uliojaa roho mbaya na chuki za makusudi uliofanywa na mtu anayejiita Kiroba kwenye mtandao wa Jamii forums.

Star TV hufaya kipindi cha Medani za Siasa kwa wanasiasa mbalimbali kila wakati. Katika vipindi vyao, huongea na 

mwanasiasa wanayemchagua kwa wakati huo na humuuliza 
mambo mengi yanayomuhusu na mambo yake ya siasa.

Ndivyo ilivyotokea kwangu weekend iliyopita.

Katika kipindi hicho, niliongea mengi kwa kujibu maswali ya mtangazaji.

Swali mojawapo aliloniuliza ni UFAFANUZI WANGU KUHUSU TUHUMA KUWA NINAMILIKI NYUMBA YA KIFAHARI.

Jamani watanzania wenzangu, nashauri sana katika masuala kama haya tuwe na utaratibu ufuatao:-
1. Kama hujaelewa au kumsikia aliyesema, basi uliza kuliko kuanza kupotosha makusudi
2. Tujitahidi kuweka pembeni siasa, hasa linapokuja suala kama hili ambalo ukweli unapatikana kwa mhusika.

Kwa kuzingatia hayo, nilichosema Star TV ni kuwa nina mkopo wa nyumba, ambayo iko hapa Dar. Bado sijaanza kuimiliki nyumba husika kwani hati bado sijakabidhiwa kwani mkopo bado sijamaliza kulipa benki. Kwa sasa, ownership ya nyumba ni ya benki.

Nimeeleza ilivyofanyika transaction husika, kuwa nilikopa 290m ndizo nilizolipa.

Wapo wanaouliza nilitoa wapi,jibu rahisi tu, ni mkopo wa kibunge ambao kila mbunge anakopa.

Wapo wanaonidhalilisha kwa kusema kuwa nimekuwa Waziri Miaka miwili na kuteneneza fedha, wananionea. Nimekuwa mbunge kwavipindi viwili, na kabla ya kuwa mbunge nilikuwa na kazi na maisha mazuri tu. Niligombea ubunge mwaka 2005 nikiwa namiliki nyumba tayari, gari 2 na mshahara mnono kwa wakati huo ulikuwa unazidi Tshs 1.5m, na cheo changu nilikuwa Mkurugenzi wa fedha na Rasilimali watu.

Sikutoka chuo na begi la vyeti kwenda kugombea ubunge. I had my life already.

Jingine kubwa tunapojadili mambo ya watu tujitahidi kukumbuka na kujiridhisha kuhusu LIABILITIES pia. Balance sheet ya mtu ina pande mbili, assets na liabilities, siyo assets tu. 

Kwa taarifa yenu, nina madeni ya kufa mtu.

Nadhani mmenielewa.

Maige
---
via Facebook
Next Post Previous Post
Bukobawadau