Bukobawadau

BALAA:MOTO WATEKETEZA NYUMBA YA MDAU MAMA PAMBA BUKOBA

Sehemu ya ya Nyumba ya Mdau Mama Pamba iliyopo Rwamishenye Bukoba usawa wa barabara kuu  ya Kibeta ikiwa imeteketea kwa moto
 Awali ya yote ashukuriwe Mwenyezi Mungu kwani hakudhurika mtu katika ajali hii"moto umeanzia  katika chumba kimoja ambacho hakikuwa na mtu
 Bi Ashura pichani shuhuda aliyenusurika katika janga hili 
Moja ya chumba kikiwa kimeteketea kabisa.
  Vitu mbalimbali vya ndani vikiwa vimeteketezwa na moto mkubwa ambambo chanzo chake hakijafahamika.
 Mshikamono wa wananchi jirani na tukio na kikosi cha zimamoto wameweza kusaidia kiasi chake

Hili ndilo balaa la janga la moto, linaloweza kutokea popote na humkuta yeyote na Hasara yake, haimithiliki kwa kuwa hukugharimu vyote ulivyochuma maishani kama inavyo onekana pichani
Hivi ndivyo inavyo onekana sehemu ya jikoni.
Mwanzo wa tukio majira ya saa 8 usiku wa kuamkia leo Ijumaa Feb 21,2014.
 Hali halisi kwa ndani kutoka na janga la moto
Bibi mkubwa wa familia ambaye amenusurika katika tukio hili.
Sehemu ya vitu vilivyo okolewa.
Baadhi ya vitu vilivyosalimika.
 Ukweli kutoka kwa Bibi huyu aliyenusurika ni kwamba watu wamejaribu kusaidia lilitokeapale linapotokea janga hili kabla zima moto awajafika ambapo anawashkuru sana kuweza  kujitahidi kwa kiasi kikubwa
Taswira iliyo nyumba hii Maeneo ya Rwamishenye barabara kuu inayoelekea Muleba.

Next Post Previous Post
Bukobawadau