CHADEMA YATOA FOMU MRITHI WA DR MGIMWA
Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza kutoa fomu za uchaguzi mdogo
Jimbo la Kalenga, mkoani Iringa huku kikijinadi kuibuka na ushindi
kwenye uchaguzi huo utakaofanyika Machi 16.
Uchaguzi huo unafanyika ili kujaza
nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Dk William
Mgimwa aliyefariki dunia Januari Mosi, mwaka huu Hospitali ya Kloof
Medi-Clinic nchini Afrika Kusini alikokwenda kwa matibabu ya figo.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni wa Chadema, Kigaila Benson alisema fomu zimenza kutolewa kuanza Februari 5 na kazi hiyo itasitishwa Februari 9, saa 10:00 jioni.
Benson alisema upigaji kura za maoni utafanyika Februari 10 mwaka huu, siku itakayofuata Kamati ya Utendaji ya Jimbo itapitia maoni yaliyotolewa na kura za maoni kisha itapeleka Kamati Kuu ya Chama yenye jukumu la kumteua mgombea.
"Febriari 12 mwaka huu, Kamati Kuu itakutana na siku hiyo tutamtangaza mtu ambaye atapeperusha bendera ya chama chetu, siku tutakayozindua kampeni na bajeti nzima itakayotumika," alisema. Chanzo: mwananchi