Bukobawadau

JINSI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO

Habari za leo Mdau,Nimeona nikupe update ili watu wa ulimwengu wa tatu tujue jinsi ya kukabiliana na changamoto.
Pichani  ni dalala maarufu hapa Manila City Philippines. Hii ni nchi inayo endelea kama Tanzania na yenye hali ngumu ya kiuchumi na idadi ya watu milioni 100.
Baada ya hali ya maisha kuwa ngumu hususani tatizo la usafiri waliamua kujitengenezea magari ya abiria (daladala) kwa kutumia mabati ya kuunga unga na chasisi. Kwa kuwa hawana technolojia ya kutengeneza injini, wananunua injini chakavu toka japan na kuunga hadi kupata daladala. Serikali iliamua kuwaruhusu kama njia kuunga mkono jitihada za wananchi. Baada ya kuhojiana na mmoja wa dreva wa magari hayo, alisema hawana njia nyingine tofauti na kubuni njia ya kujinasua kwenye tatizo la usafiri kwa kuchonga magari hayo. Baada ya kufanya utafiti nimekuta nje gari inanembo ya benzi injini Mitsubishi, nyingine nje inanembo ya Mitsubishi ndani injini ya Hilux. Pia magari hayo hayana milango wala hawajali uzuri(shape ya gari) wanajali huduma . Pia ni jambo la kawaida dreva kuendesha akiwa kifua wazi 


Umaskini ni kitu kibaya, umbali uliopo kati ya Manila na Japan ni masaa matatu angani lakini wanashindwa kununua gari original toka Japan.
By Ahmed Issack
From Manila - Philippines
Next Post Previous Post
Bukobawadau