LEO KATIKA KUMBUKUMBU MWAKA 1997 KIKOSI CHA RTC KAGERA CHAIZUIA SIMBA KUTWAA UBINGWA.!!
Leo katika kumbukumbu na Bukobawadau Blog, Mwaka 1997 michuano ya ligi kuu tanzania bara ikiwa
ukingoni kabisa ambapo mchezo wa mwisho ulifanyika Mjini hapa ndani ya uwanja wa kaitaba
kati ya Simba Fc v/s RTC Kagera maarufu kama Wagadi, Simba ilihitaji
ushindi ili ibebe kombe,lakini mambo yalienda ndivyo sivyo wakapokea
kichapo cha mabao 3-1, kutoka kwa kikosi mahiri cha wachezaji wa RTC Kagera.
Kumbukumbu zinaonyesha wachezaji wa timu ya RTC waliokuwa wamekalia benchi chini ya Kocha wao Mzee Sonday Kayuni kama/sub ni Bure Mtagwa, Issa Ally, Zahoro Sabuu( check bob),marehemu Mukama Ntale,Patric Oswin,Mustapha Simba,Albert Sengo, mtu wa skendo kwa nyakati hizo Salmin Kamau na Endrew Kabaya.
Ushindi ulipatikana kupitia mikakati na mbinu pamoja na ushirikiano kati ya RPC wa Mkoa kipindi hicho Marehemu Jumbe na Mkuu wa Mkoa aliyekuwepo Mzee Mangula.
Kikosi kamili uwanjani ni kama ifuatavyo.

- ONESMO EDWARD
- ABDUL KITUMBA
- JOHN FAYA
- ABUU OMARY
- GODWINI KICHEMU
- OMARY SAID
- MOVISHA HAULENA
- KASIGA MACHAPATI
- CLEMENT KAHABUKA
- FULGENCE NOVATUS
- MUSSA MASSARO