MACHACHE KUTOKA BUNGENI LEO FEB 20,2014
Kutokana
na bunge kutokuonywesha ama kutangazwa kwenye vyombo vya habari,
wananchi tumekua tukipata habari kidogo na za kudokoa dokoa. Kwa kupitia
social media nyingine kuna wajumbe wamekuwa wakihabarisha kiasi nini
kinaendelea kwenye bunge hilo maalum.
Haya ni baadhi ya niliyopata toka kwenye tweets za mjumbe Maria Sarungi.
- Wabunge wataka posho ziongezwe, wanataka Ipad badala ya karatasi.
-"Tuachane na posho tupo kwenye kupitishwa rasimu ya kanuni na sheria ya mabadiliko" - AG Werema
- Mwenyekiti wa muda wa Bunge La Katiba ameunda kamati ndogo ya wajumbe 6 kuchunguza suala la malalamiko ya posho juu ya bunge hilo la katiba. Wajumbe wanaounda kamati ya kuchunguza posho ni Lukuvi, Freeman Mbowe, Paul Kimiti, Mohamed Aboud, Asha Makame na Jenista mhagama.
- Vikundi vya kijamii na NGOs imewakilishwa na Paul Kimiti katika kamati maalum ya Posho
- Kanuni za bunge zimepitiwa, zikiwa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza. Kanuni hizo zikipitiwa na kupitishwa na wajumbe wa baraza la Katiba, ndipo shughuli rasmi za Bunge la Katiba zitaanza.
- Tundu Lissu aliomba ufafanuzi wa kifungu 9 na 25 kwamba hazina uhusiano.
- Zitto aliomba ufafanuzi kama Rasimu mbadala ina nafasi ya kujadiliwa
- Mwalimu Oluoch alizungumzia tofauti ya tafsiri ya kifungu 25 kwa kiingereza na kiswahili. Kuna maneno hayatafsiriwa kwa Kiswahili.
- Bado ufafanuzi kwa nini Bunge la Katiba halionyweshi kwenye TV
- (Tetesi) za kuwepo katiba mbadala iliyo andiwa na kikundi kisichojulikana.
-Ismail Jussa aliomba ufafanuzi wao kwama wajumbe (yaani Delegate) si wabunge - wanaruhusiwa kugusia rasimu hii kutokana na maoni ya wananchi?
- "Bunge maalum isinyang'anye madaraka ya rasimu inayotokana na maoni ya wananchi" - Lipumba
- Ismail Jussa alisoma vifungu vya 25 kwa kiingereza na kiwahili akiomba ufafanuzi. 25 (2) pia ameeleza 'shall be exercised by Bunge la Katiba'
- Jaji Werema alieleza kuwa kama kuna rasimu mbadala isomwe lakini haiwezi kutumika kama msingi wa mjadala
- Jaji Werema alieleza kuwa rasimu iliyotokana na maoni ya anachi ndio itatumika kuboresha. Rasim mbadala ni maoni tu.
- Jaji Werema alieleza rasimu iboreshwe lafu irudi kwa wananchi kwa kura za maoni.
Baadhi ya maoni ya Maria Sarungi juu ya posho.
Wananchi suala la posho la wajumbe wa #BungeKatiba mwambieni rais
@jmkikwete asiongeze hata senti tano .. mi shatuma ujumbe
#ChangeTanzania
- @gracemacha nasema hivi rais
@jmkikwete asiongeze posho itangazwe na wajumbe wasioafiki wasimame na waseme tuwajue
@Tanzania_Kwanza
-Kitu ninachotetea ni wale wajumbe wanaokuja na wasaidizi. Ila ilitangazwa kuwa wasaidizi watalipwa posho yao separate.
#BungeKatiba
-Nilishasema wazi posho ya kujikimu na posho maalum ya sasa inaweza isitoshe ukitaka kuishi maisha fulani. Ni lazima kubadili matarajio.