Skylight Band yazidi kukonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya kiota cha Thai Village
Kikosi kazi cha Skylight Band kikiongozwa na Joniko Flower wakitoa burudani kwa mashabiki wao Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Kikosi kazi cha Skylight Band kikisebeneka jukwaani.
Hashim Donode wa Skylight Band (katikati) akitoa burudani kwa wapenzi wa bendi hiyo ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar. Kulia ni Winfrida Richard na kushoto ni Digna Mbepera.
Pichani juu na chini ni mashabiki wa Skylight Band wakijimwaga kwenye dancing floor ndani ya ukumbi wa Thai Village Masako jijini Dar.
Mashabiki wa Skylight Band wakicheza miondoko ya "Yachuma chuma" kwenye show iliyobamba vilivyo ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Muguu wa kushoto mbele, wa kulia nyuma......mi nataka mukanda yachuma chuma weeeee.....!!!!
Aneth Kusbaha AK47 na Winfrida Richard wakitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band.
Katika kupata ladha nzuri ya muziki wa Skylight Band vijana hawa ndio wanahusika asilimia 100. Pichani juu ni Moses na chini ni Athumani pamoja na Idrissa wakinya yao.
Umati wa wadau wa Skylight Band wakiburudika na muziki wa Bendi hiyo Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Digna Mbepera akifanya yake jukwaani.
Mambo ya pwani yalihusika pia....Chezea mduara weweeee...!!!
Mwanafamilia wa Skylight Band Victor Maginga (wa pili kushoto) akipata ukodak na marafiki zake ndani ya kiota cha Thai Village Ijumaa iliyopita.
Mdau John Mwansasu (mwenye shati jeusi) akiwa na rafiki yake.
Alfio wa Ogopa Video's akishow love Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village.... Skylight Band wamefanya shooting ya moja ya nyimbo zao ni ipi kaeni mkao wa kula soon utaiona kupitia Luninga yako.
Aneth Kushaba AK47 akishow love na fans wake back stage.
Picha juu na chini ni mashabiki wakubwa na wadau wa Skylight Band wakipata Ukodak.
Mdau Alois Ngonyani(kushoto) akishow love na mdogo wake.