Bukobawadau

VALENTINE SPECIAL-FEB 14, 2014

Hakuna hata mmoja asiye na mapungufu kwenye mahusiano, tukiamua kuangaliana kwa kuchunguzana makosa na mapungufu yetu basi kila mmoja atajikuta hakumstahili mwenzake. Nikweli kabisa kwamba makosa na mapungufu yanaumiza, tena sana, lakini kamwe usiyaruhusu yawe ndiyo kioo cha kumtazama mwenzako. Naamini kuna mema na mazuri machache amewahi kuyafanya, naamini hatakama amekuumiza, na akakufanya ukalia, kuna nyakati pia alikufanya ukacheka, kwanini sasa usiweke mtazamo wako katika hayo mema badala ya kupoteza muda na nguvu zako kuwaza hayo mabaya? Usimtazame kama hakimu anavyomtazama mshtakiwa, mtazame mpenzi wako kama ambavyo Mungu anamtazama
 KWA WANAWAKE WALIOKO MAHUSIANO
 

Haijalishi unaheshimiwa, kujaliwa na kuaminiwa kwa kiasi gani na watu wa ofisini au kazini kwako au wote walioko nje ya nyumbani kwako. Heshima hizi, kujaliwa huku na kuaminiwa huku kamwe hakutokuridhisha au hata kuugusa moyo wako kwa namna yoyote kama bado mpenzi wako (mume wako) hakujali, hakuheshiku na hakuamini. “Always charity starts at home”. Mwanamke mmoja aliyekuwa Rais wa shirikia kubwa la ndege ulimwenguni na aliyeheshimika sana aliwahi kujibu hivi “……baada ya haya yote, mwisho wa siku kilicho muhimu zaidi kwangu ni pale ninapofahamu kuwa mume wangu ananipenda, ananijali na kuniheshimu, hiki ndicho cha muhimu zaidi kwangu kuliko kingine chochote”. Fungua macho yako na utazame kwenye mahusiano yako leo, unapanda nini? na unavuna nini? Au unataka kuvuna pasipo kupanda? 

JE UTAUMIZWA MPAKA LINI?

Mwanamke! Yakusaidia nini kutafsiri kila tendo analokutendea mwanaume kuwa ni penzi wakati hata yeye bado hajatamka chochote? Yamkini ameamua kukupa, au kukufanyia, au kukusaidia kitu fulani kwa mazingira fulani, kwanini utafsiri kuwa kwa kufanya vile kasukumwa na penzi kwako? Halafu ukishawaza hivyo unajirahisisha na kujiachia ukizama kwenye dimbwi la fikra kuwa unapendwa na kupenyeza mizizi ya penzi ambalo mkandarasi ni wewe pekeyako. Mara unapojirahisisha nayeye kwa kushindwa kuvumilia akaamua kutumia fursa kujiliwaza na baadae akaamua kuondoka kama alivyokuja unaanza kulaani na kulia kwa sauti, sasa hapa wa kulaumiwa ni nani? Kwanini kujitengenezea mazingira ya mahusiano yenye sumu? Kama amefanya tu na hajasema kitu basi bado hujapendwa, na hata kama akisema kitu, kwanini usisubiri kuona kama kilichosemwa kinaendana na yanayofanywa? Usisahau kwamba katika mahusiano matendo yanayoonyesha penzi “hayatafsiriwi tu” bali yanaonekana DHAHIRI

 
Next Post Previous Post
Bukobawadau