AL-SHABAB LATANGAZA MAUAJI KUPITIA FACEBOOK
Kundi
la wanamgambo wa Somalia Al-Shabab limesema limewaua watu watatu ambao
linawashutumu kufanya upelelezi katika mashirika ya kijasusi ya Marekani
au Somalia. Kundi hilo lenye uhusiano na al- Qaida lilitangaza mauaji
hayo Jumanne katika ukurasa wake wa Facebook.
Limesema
mmoja wa wanaume waliouawa mwenye umri wa miaka 29 Mohamed Abdulle Gelle
aliongoza ndege isiyokuwa na rubani ya Marekani kufanya shambulizi
lililouwa kamanda wa Al- Shabab katika mji wa Juba nchini Somalia Oktoba
mwaka jana.
Hilo likiashiria shambulizi lililomuuwa mtaalamu wa milipuko wa Al- Shabab aliyejulikana kama Anta, mwezi oktoba 28 mwaka jana.
Al-Shabab
lilisema mtu wa pili, Ahmed Abudllahi Farole mwenye umri wa miaka 47
alifanya ujasusi kwa niaba ya serikali ya jimbo la Puntland. Mwanamume
wa tatu ambaye hakutambulishwa, alishtumiwa kwa kufanya ujasusi kwa
niaba ya serikali ya Somalia.
Taarifa hiyo ilisema wanaume hao watatu walipigwa risasi na kikosi cha walenga shabaha katika mji wa Barawe.
CHANZO:VOA