Tamko
hilo la kusitisha maandamano hayo limetoleo mara baada ya baadhi ya
viongozi wa juu wa timu hiyo kukutana na viongozi wa serikali.
Viongozi
hao wa serikali walitoa tamko kuhusu kushughulikia ombi lao hali
iliyosababisha viongozi wa Yanga kusitisha maandamano yao waliyokuwa
wameyapanga kuyafanya juma hili.
Juma
lililopita Katibu wa baraza hilo, Ibrahim Akilimali alitoa siku tano
kwa Baraza la Madiwani Manispaa ya Ilala, liwe limewapa kibali cha
ujenzi huo, vinginevyo waliahidi kufanya maandamano makubwa.
Amesema
viongozi wa juu wa klabu hiyo walikutana na viongozi wa serikali
akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadik Mecky Sadik, Meya wa Ilala
Jery Silaa na Diwani wa Kata ya Jangwani ambapo walikubaliana ombi lao
kufanyiwa kazi.
Akilimali
amesema serikali kupitia Manispaa ya Ilala ilieleza kuwa ombi lao
linashughulikiwa kwa haraka, hivyo aliwataka wanachama wa klabu hiyo
kuelewa jambo hilo bila kuwepo na migogoro.
Ameweka
wazi kuwa wanaamini serikali kupitia Manspaa ya Ilala watalishughulikia
ombi lao, ingawa amesisitiza kuwa ikitokea ombi lao hilo
linaloshughulikiwa likija na majibu ya “hapana” watatafuta mbinu
nyingine.
"Sisi
tumeomba hivyo majibu ni mawili ndiyo tumepata au tumekosa, ikitokea
likaja jibu la kukosa hapo ndiyo kutakuwa na utata na kuamua cha
kufanya," alisema katibu huyo wa baraza la wazee wa klabu ya Yanga.
Ameongezea
kuwa klabu hiyo imejiandaa kuwalipa watu waliongezeka katika eneo lao,
hivyo hawaoni sababu za kwenda kujenga nje ya mji wakati wao ni watoto
wa mjini.