Bukobawadau

HAPPY BIRTHDAY BABA ASKOFU METHOD KILAINI

 Leo Jumapili Marchi 30,2014  ni siku ya kipekee kwa Baba Askofu Method Kilaini kwa kufikia tena tarehe ya kuzaliwa kwake.Happy birthday kwako Baba Askofu Method Kilaini,tunazidi kukuombea  ili Mungu aendelee kukutumia kuwaongoza wanadamu kumuelekea muumba wao.

 Baba Askofu Method Kilaini amezaliwa Katoma Bukoba 30 Machi 1948. Aliwekwa wakfu na kardinali Agnelo Rossi mwaka 2000. Tangu hapo hadi 2009 alikuwa askofu msaidizi wa jimbo kuu la Dar es Salaam, halafu akahamishwa kuwa askofu msaidizi wa askofu wa Jimbo la Bukoba.
Askofu Kilaini alipewa upadrisho Roma mwaka 1972 na Kardinali Angelo Rossi baada ya kupata shahada ya pili ya Teologia jijini Roma. Baada ya kurudi nyumbani Bukoba Tanzania alifanya kazi parokiani, baadaye alikuwa mhazini msaidizi wa jimbo. Kati ya mwaka 1978 hadi 1985 alifundisha Historia ya Kanisa katika Seminari Kuu ya Ntungamo. Mwaka 1985 alirudi Roma na kupata shahada ya udaktari wa tauhidi katika Historia ya Kanisa kutoka chuo Kikuu cha Gregoriani mwaka 1990.
 

Mwaka 1990 hadi 2000 alikuwa Katibu mkuu wa baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania. Kuanzia mwaka 2000 alikuwa askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam hadi mwaka 2009 alipoteuliwa kuwa askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba. 

 BUKOBAWADAU BLOG TUNAKUTAKIA MAISHA MEMA YENYE BARAKA SIKU ZOTE ZA MAISHA YAKO!!!




Next Post Previous Post
Bukobawadau