HAWA NDIYO NDEGE AINA YA NYANGENYAGE WANAOZUA KIZAAZAA KATIKA KISIWA CHA MUSILA ZIWANI VICTORIA MANISPAA YA BUKOBA MKOANI KAGERA
Jamani Katika Kisiwa Kiitwacho
Musila Hali ni tete kutokana na Ndege aina ya Nyange Nyange Kukivamia kisiwa
hicho na kutishia maisha ya wakazi waishio katika kisiwa hicho wapatao 536.
Pichani Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe alipotembelea kisiwa cha Musila
Pichani Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe alipotembelea kisiwa cha Musila
Aidha ndege hao wanakunya ovyo na
kusababisha harufu mbaya mavi yao kutoboa mabati, pia wameua mbuzi 12, kuku 512
wamekufa, na kusababisha watu kuhara na kuharisha mara kwa mara nawakati
mwingine kujisikia kuishiwa nguvu.
Pamoja na Hayo yote Kisiwa cha
Musila kinachokaliwa na wananchi 536 bado walikuwa hawana vyoo hata kimoja
jambo ambalo lilimfanya Mkuu wa Mkoa kutoa wiki moja kila kaya kuchimba choo
chake.
Agizo hilo lilitekelezwa na
wananchi hao kwa kuchimba vyoo 30 katika kisiwa hicho. Mkuu wa Mkoa pia
amewaagiza kuandaa vifaa vya ujenzi visivyokuwa vya viwandani ili wajengewe
shule na Zahanati katika kisiwa Hicho.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Inaendelea na utafiti kuhusu kinyesi cha ndege hao kuona kama kina madhara jkwa
binadamu. Sampuli za kinyesi cha wananchi wa Musira kilichukuliwa ili
kuchunguzwa kama kuna madhara yatokanayo na ndege hao.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2014