KWA WAKINA DADA MLIOKO KWENYE MAHUSIANO
Yamkini
umeshasikia usemi usemao “mbinu bora ya kuondokana na mwanaume
uliyemchoka ni kutafuta mwanaume mwingine” sawa naweza kukubaliana na
wewe, lakini jiulize, je kule kuondokana na huyo unayetaka akuache
kunakufanya uwe salama na mwenye furaha? Yamkini unaifuata ile methali
isemayo “dawa ya moto ni moto” lakini nikutahadharishe tu kwamba sio
methali zote zinatenda kazi kwenye
mahusiano kama vile zilivyo, ziko nyakati kwenye mahusiano dawa ya
kuzima moto siyo kuwasha moto mwingine bali ni kumwaga maji, tena ya
baridi kabisa. Usije kuwa na misimamo ambayo itayafanya macho yako
yasikauke machozi kwa jinsi utakavyodumu kwenye kulia kwa kuumizwa moyo
kila wakati, kwasababu mwisho wa siku utajikuta umekuwa mtaalamu wa
kumiliki wanaume wasiokaa. Sasa sijui wote waliopita kwako na ukawaacha
uliwapenda? au ndiyo walikuwa wanapita kama wafanyakazi kwenye usahili
“interview”!