Bukobawadau

MKUTANO WA WAZAZI KUINUA TAALUMA HUKO KANYIGO KIKUKWE SEKONDARI


Pichani wazazi wakisikiliza kwa makini wakati wa mkutano,kulia anaonekana mmoja wa Wazazi Ndg Deogratias Bunyomyo akichangia mawazo wakati wa mkutano

Wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Kikukwe wakiwa darasani,picha ya pili ni baadhi ya walimu sekondari ya Kikukwe
  NA MUTAYOBA ARBOGAST,Missenyi
MKUTANO wa  wazazi katika shule ya sekondari Kikukwe kata ya Kanyigo
katika mkutano uliofanyika leo shuleni hapo umefikia uamuzi wa
kuchangia kila mzazi kuchangia sh 22,000 kwa wanafunzi wa kidato cha
kwanza na cha tatu na wazazi wenye watoto kidato cha pili na nne sh
25,000 ikiwa ni fedha ya ziada ya kuinua taaluma shuleni hapo.

Aidha wazazi wamekubaliana kuwa wote kwa pamoja washirikiane kuangalia
nidhamu ya wanafunzi nje ya shule hata kama mtu si mtoto wake mwenyewe
na waache tabia ya kuwatuma watoto shughuli za biashara ,wanafunzi
kuhudhuria misiba isiyowahusu,na kuwa mzazi atakayehusika
kumsababishia utoro mtoto wake,hatua kali zichukuliwe dhidi yake na
kama ni utoro wa mtoto mwenyewe uripotiwe shuleni
Hatua hizo na nyingine ni makubaliano ya kuinua taaluma ambapo matokeo
ya waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2013 yamekuwa daraja la
kwanza(1),la pili(2),la tatu(0),la nne(11)na daraja 0(44).
        
Mkuu wa shule hiyo Alisen Laurent amesema amejipanga na walimu
wenzake kuewka mikakati ya ufaulu kwa kuwapanga katika makundi ya
ufaulu waliyojichagulia wanafunzi ili wawe na hamasa(wanafunzi)ya
kufikia malengo waliyojiwekea.
Hata hivyo amesema shule ina uhaba mkubwa wa walimu wa Sayansi na kuwa
atatumia mchango wa taaluma kujaribu kupunguza tatizo hilo.Shule ina
wanafunzi 248 na walimu walioajiriwa 12.

picha:mkuu wa shule,Alisen Laure akitoa hotuba yake na
wanaomfuatia-wenye makabrasha ni mwenyekiti wa bodi ya shule,mchungaji
Felix Rwabyo na afisa mtendaji kata ya Kanyigo,Juma Swaibu

Next Post Previous Post
Bukobawadau