RATIBA YA MKUTANO WA BUNGE MAALUM TAREHE 17 HADI 21 MACHI, 2014
BUNGE MAALUM
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RATIBA YA MKUTANO WA BUNGE MAALUM TAREHE 17 HADI 21 MACHI, 2014
Ofisi
ya Katibu wa Bunge Maalum inawatangazia Wajumbe wa Bunge Maalum na umma
kwa ujumla kuwa Mkutano wa Bunge Maalum utaendelea mjini Dodoma Leo
kwa ratiba ifuatayo:
Tarehe 17/3/201 kuanzia saa 3:00 asubuhi kutakuwa na kiapo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum ambao bado hawajaapishwa.
Hivyo
Wajumbe wote ambao hawajaapa kiapo cha ujumbe wa Bunge Maalum
wanatangaziwa kufika Idara ya Shughuli za Bunge Maalum kesho saa 2:00
asubuhi bila kukosa kwa ajili ya kutambuliwa.
Saa
11:00 jioni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph
Sinde Warioba atawasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum.
Tarehe
18/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi Wajumbe wote wa Bunge Maalum
watapewa semina kuhusu ufahamu mpana zaidi wa Kanuni za Bunge Maalum.
Tarehe
19 na 20/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi wajumbe wote watapewa semina
kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania.
Tarehe
21/3/2014 saa 3:00 asubuhi kutakuwa na uteuzi wa Wajumbe wa Kamati za
Bunge Maalum na saa 10:00 jioni Mgeni Rasmi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania atalihutubia Bunge kuashiria ufunguzi rasmi wa
Bunge Maalum
Atakaye ipata taarifa hii amjulishe mwenzake.
Imetolewa na Ofisi ya
KATIBU WA BUNGE MAALUM