Skylight Band yaendelea kuwapa raha mashabiki wake, ni Ijumaa hii tena @ Thai Village
Vijana wa Skylight Band wakitoa burudani Ijumaa iliyopita kwa mashabiki wao kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar... Burudani inaendelea kama kawaida tukutane tena leo jioni......ni balaaaaa..!
Divas wa Skylight Band... Kutoka kushoto ni Digna Mbepera, Mary Lucos na Aneth Kushaba AK47 wakikonga nyoyo za mashabiki wao ndani ya kiwanja chao cha nyumbani Thai Village Ijumaa iliyopita.
Mashabiki wa Skylight Band wakijimwaga kwenye dancing floor.
Rapa Joniko Flower akiongoza kikosi cha Skylight Band kutoa burudani ya aina yake Ijumaa iliyopita.
Mbwembwe za mashabiki wa Skyight Band pale burudani inapokolea watu humwaga radhi.
Kwa raha zao huku burudani ikiendelea.
Mpiga Tumba wa Skylight Band Daudi akifanya yake jukwaani...!
Hela yako haipotei bure kwa burudani kama hii... ni balaaa...!
Sam Mapenzi akipagawisha mashabiki wa Skylight Band ndani ya kiota cha Thai Village Ijumaa iliyopita...Pichani ni mdau Alois Ngonyani akionekana kukunwa na uimbaji wa kijana Sam Mapenzi.
Sam Mapenzi a.k.a asali ya warembo akiburudika na mmoja wa mashabiki wa Skylight Band.
Muziki wa pwani a.k.a mduara ulihusika pale kati.
Mashabiki wa Skylight Band wakijimwaga na mduara.
Palikuwa hapatoshi hapo kati.
Wadau wa Skylight Band wakishow love na Ukodak.
Mwanafamilia wa Skylight Band Victor Maginga (kulia) akiwa na DJ Peter Moe pamoja na mdau wakipata Ukodak.
Aneth Kushaba AK47 akishow love na washirika wakubwa wa Skylight Band Alois Ngonyani (katikati) pamoja na Emmanuel Francis.