Skylight Band yatikisa jiji la Dar kwenye 'Nyama Choma Festival' ndani ya viwanja vya Posta
Sam Mapenzi na Sony Masamba wakitoa burudani ya aina yake kwenye tamasha la Nyama Choma lililofanyika Jumamosi hii kwenye vianjwa vya Posta jijini Dar ambapo Skylight Band iliongoza kwa kukusanya mashabiki lukuki.
Sam Mapenzi wa Skylight Band akishindana na mmoja wa mashabiki kucheza wimbo wa Davido SKELEWU.
SKELEWU SKELEWU SKELELEEE.......!!
Vijana wa Skylight Band wakishambulia jukwaa.
Mashabiki wakijiachia wakati Skylight Band ilipokuwa ikitumbuiza kwenye Tamasha la Nyama Choma lilofanyika Jumamosi hii ndani ya viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar.
Winfrida Richard (katikati), Hashim Donode pamoja na Digna Mbepera wakiwapa raha mashabiki wa Skylight Band kwenye tamasha la Nyama Choma ndani ya viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar.
Burudani zilikuwa nyingi kwenye tamasha la Nyama Choma lakini Skylight Band ilifunika kwenye kuteka mamia ya mashabiki.
Umati wa wakazi wa jijini Dar wakipata burudani ya aina yake kwenye tamasha la Nyama Choma wakati Skylight Band ikitumbuiza.
Mashabiki wa Skylight Band waliamua kupanda jukwaani na kuonyeshana ufundi.
Dar es Salaam are you feeling the music..........yeah......!!!
Daudi Tumba na mpiga Bass wa Skylight Band Chili Chala wakifanya yao jukwaani.
Mdau Laurean Kiiza akishusha kinywaji chake baridi...ilikuwa ni mara yake ya kwanza kushuhudia Live Performance ya Skylight Band na sasa ameahidi kuwa mdau mkubwa wa Bendi hiyo.
Ukizingatia ilikuwa ni siku ya Wanawake Duniani walipataje raha na Skylight Band....!
Mtaalam wa Nyama Choma akifanya yake ndani ya viwanja vya Posta.
Kuku wakiwa kwenye hatua za maandalizi.
Familia ya Skylight Band ikiongozwa na Mkurugenzi mkuu wa Band hiyo Dr. Sebastian Ndege.
Mmilikiwa Duka la Zuri Fashion Boutique, Fashionista ambaye pia ni Blogger dada Jestina George akishow love na shemeji yake kwenye Nyama Choma Festival iliyofanyika kwenye viwanja vya Posta.
When Bloggers meet! Operations Manager wa MOblog Zainul Mzige akipata ukodak na Blogger Jestina George...hawa jamaa walikuwa wakiwasiliana kwa njia ya barua pepe katika kupashana habari, hatimaye walikutana uso kwa uso kwenye Nyama Choma Festival ndani viwanja vya Posta.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau walihudhuria Nyama Choma Festival iliyofanyika Jumamosi hii kwenye viwanja vya Posta jijini Dar.
Mzee wa Skonga ya EATV Allan Lucky akishow love na warembo ndani ya Nyama Choma Festival.
Mrs. Lucky pamoja na wifi yake.
Mdau Emmanuel akishow love na mrembo wa ukweeeh ndani ya viwanja vya Posta.
Model Danny David pamoja na Noel Ndale wakipata Ukodak kwenye Nyama Choma Festival.
Noel Ndale akishow love na mrembo kwenye band la Jack Daniel's.