SKYLIGHT BAND YAZIDI KUWAKUNA MASHABIKI WAKE NDANI YA KIOTA CHA THAI VILLAGE
Waimbaji wa Skylight Band kutoka kushoto Hashim Donode, Digna Mbepera, Winfrida Richard na Aneth Kushaba AK47 wakitoa burudani kwa mashabiki wao Ijumaa iliyopita kwenye uwanja wao wa nyumbani Thai Village Masaki jijini Dar...Ni Ijumaa zote wako Thai Village bila kusahahu Jumapili kwenye Family Day Bonanza ndani ya kiota cha Escape One Mikocheni.
Raia wa kigeni (Watasha) wakionekana kuchizika na burudani ya Skylight Band.
Hashim Donode na Winfrida Richard wakifanya yao jukwaani.
Winfrida Richard akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Ban (hawapo pichani) huku Aneth Kushaba AK47, Hashim Donode na Digna Mbepera wakisebeneka.
Burudani mwanzo mwisho ndani ya kiota cha Thai Village...Hapana chezea Skylight Band.
Sam Mapenzi sambamba na Hashim Donode na Sony Masamba wakikonga nyoyo za mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Na watuache kwa raha zetu... Skylight Band ndio habari ya mujini.
Mwanadada akisuuzika na burudani ya Skylight Band.
Sony Masamba na Mpiga drum wa Skylight Band Idrissa wakionesha ufundi wao wa kusakata sebene kwa mashabiki wao.
Mpiga Solo wa Skylight Band, Allen Kisso Mzuzu akifanya yake jukwaani.
Mashabiki wakifanya yao kwa dancing floor....ni raha....!
Chukua baba umeukonga moyo wangu......Sam Mapenzi akitunzwa na shabiki wake.
Mamia ya mashabiki wa Skylight Band wakisebeneka na burudani ya aina...ni Skylight Band pekee inakupa burudani adhimu kama hizi.....!!!
Watu weweeeeeeee ngoma inogile....Skelewu.....Skelewu......!!
Naitwa Aneth Kushaba AK47 na hizi ndio swagga zangu...Njoo leo tuimbe na kucheza wote ndani ya Thai Village Masaki jijini Dar.
Jambo Tanzania....We are number one fans of Skylight Band...!