Bukobawadau

VITUKO VYA WANANCHI BAADA YA GARI LA BIA KUANGUKA MAENEO YA KEMONDO JIONI YA LEO MARCHI 1,2014

Ni ajali  iliyotokea jioni ya leo Jumamosi marchi 1,2014 majira ya ya saa kumi alasiri ambapo gari gari aina ya Semi Trela mali ya kampuni ya Zachwa Investment ya Mjini Bukoba   lililokuwalimesheheni sanduku za chupa za bia zenye vileo kuanguka katika kijiji cha Kemondo.
Wanakijiji walivamia gari hilo baada ya kugundua nini kilichomo
 Hakuna kifo kilichotokea  baada ya gari lililokuwa limebeba sanduku za bia zenye pombe kuanguka.
Licha ya kontaina  la gari kuwa limefungwa bado wananchi walifanya mikakati yao kwa kuchimba Shimo ili  maji ya bia yaweze kuingia .
 Baada ya hapo ikawa kama sherehe kwa wanakijiji 
 Wakazi wa Kijiji cha kemondo wakipata kinywaji cha bwelele.
Hiki ndicho kilichotokea baada ya Gari la bia kuanguka na wanakijiji kukusanyika na kushambulia  kinywaji kilichokuwa kinatiririka  kufuatia kupasuka kwa chupa za bia katika ajali hiyo.
Next Post Previous Post
Bukobawadau