Bukobawadau

YANGA YAONDOLEWA MASHINDANO YA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA KWA PENATI

Young Africans imetolewa kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika na mabingwa watetezi Al Ahly kwa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia kumalizika kwa dakika 90 za mchezo Al Ahly ikiwa na bao 1- 0 hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 1-1 mchezo uliofanyika usiku wa leo katika Uwanja wa El Max jijini Alexadria.
Young Africans iliingia uwanjani ikiwa makini na kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa lango la Al Ahly lakini Didier Kavumbagu alishindwa kutumia nafasi hiyo na mpira kuokolewa na walinzi kabla ya kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Al Ahly walifanya mashambulizi langoni wa Young Africans lakini walinzi wake Kelvin Yondani, Nadir Haroub walikua makini kuokoa michomo hiyo huku mlinda mlango Dida akifanya kazi za ziada kuokoa hatari lanongi mwake.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Al Ahly 0 - 0 Young Africans.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mashambulizi na kusaka mabao ya mapema lakini bado ngome zote zilikuwa makini na kufanya milango kuwa migumu huku mwamuzi wa mchezo leo kutoka nchini Sengal akiwaonyesha kadi wachezaji wa Yanga na kupuliza filimbi kila wachezaji wa Al Ahly walipogiswa.
Dakika ya 70 ya mchezo mlinzi wa kushoto wa Al Ahly Saed Mowaeb aliipatia timu yake bao kufuatia mpira alioupiga kumzidi uwezo mlinda mlango Deo Munish na kujaa wavuni na kuhesabu bao.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Al Ahly 1 - 0 Young Africans hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa 1-1 kufuatia Yanga kushinda bao 1-0 pia jijini Dar es salaam.
Mara baada ya kumalizka kwa dakika 90 mwamuzi aliamuru zipigwe penati ambapo wapigaji wa Young Africans waliopiga ni
Nadir Haroub - alifunga
Didier Kavumbagu - alifunga
Emmanuel Okwi - alifunga
Oscar Joshua - alikosa iligonga mwamba
Said Bahanuzi - alikosa ilitoka nje
Mbuyu Twite - alikosa iliokolewa na golikipa Ekramy
Al Ahly penati zao zilifungwa na
Abdalllah Said, Gedo, Trezeguet na Mohamed Nagieb huku mlinda mlango Deo Munshi akizipangua penati mbili za Saed Mowaeb na Hossan Ashour
Young Africans: 1.Dida, 2.Twite, 3.Oscar, 4.Cannavaro, 5.Yondani, 6.Domayo, 7.Msuva, 8.Ngasa/Chuji, 9.DKavumbagu, 10.Okwi, 11.Kizza/Bahanuzi  (P.T)
Next Post Previous Post
Bukobawadau