Bukobawadau

HUKO KANYIGO SHAMBA NA NYUMBA VYAHARIBIWA KWA TUHUMA ZA WIZI !!

WATU wasiofahamika katika kitongoji cha Katale,kijiji cha Kikukwe,kata ya Kanyigo,wilaya ya Missenyi jana majira ya saa mbili na nusu asubuhi wamefyeka shamba la migomba ekari zipatazo mbili,kubomoa nyumba ya tofali na bati na kuharibu mali nyinginezo yakiwamo mavuno ya chakula
na nguo, kwa mkazi wa kitongoji hicho,Gratian Mbelwa Ignatio wakimtuhumu kwa vitendo vya wizi.

 Katika hali ya mshangao, ndivyo anavyo onekana pichani mtoto mwanafunzi wa  darasa la kwanza mara tu aliporudi nyumbani majira ya saa tano asubuhi na kutaka mambo hali  kama hii
 Bi Eliada Mbelwa,mke wa mtuhumiwa wa wizi akiwa amesimama mlangoni mwa nyumba ya mama mkwe wake(kwenye kaya hiyo) akitafakari yaliyojili.
         “Mume wangu amerudi tu wakati wa sikukuu za pasaka,alikuwa kibaruani huko Bugabo,Bukoba vijijini kwa kipindi cha miezi mitatu.Sasa jana mtoto wa baba yake mdogo anasema eti amemuibia baiskeli yake.Yeye ameondoka leo asubuhi na mapema kurudi kazini kwake,kisha naona watu wanakuja na mapanga kwa hali inayoonesha shari hivyo ikabidi nikimbie kuokoa roho yangu,” anasema kwa majonzi Eliada Mbelwa,mke wa mtuhumiwa.
Baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho wamesema  wamechoshwa na tabia ya mtu huyo kutokana na vitendo vya wizi na kwamba kila anapokuja kijijini lazima kutokee wizi,hivyo wakaona wamfanyie hivyo asubuhi na si usiku ikiwa ni ishara ya onyo kali na asipojirekebisha watachukua
hatua zaidi.
Wakati tukio hilo linatokea watoto wao walikuwa tayari wamekwenda shuleni.

 "Watoto hucheza" ,huyu ni mtoto katika familia husika,baada ya kulia kwa muda fulani,sasa ameamua kucheza
  Hivi ndivyo shamba  lilivyofyekwa
 Taswira mabaki ya nyumba iliyoharibiwa
Mwenyekiti wa kitongoji hicho,Ndugu Hosea Mugini amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na alikuwa kwenye harakati za kulijulisha jeshi la polisi.
 NA MUTAYOBA ARBOGAST,Missenyi
Punguzo  maalum la bei katika msimu huu wa sikukuu ya Pasaka, sasa unaweza kufurahia chaneli zaidi y 70 bila dish wala chengachenga, utapata king'amuzi kwa Tsh 79,000 badala ya 109,000.wahi package yako yenye kifurushi cha Tsh 40,000 bure.
 BUKOBA fika ITEMBWE GENERAL SUPPLIES wakala mkuu wa Startimes ,wanapatikana Kashozi Road, mkabala na ofisi ya MAYAWA au piga simu namba 0787 007 666/0754 760 633.
 Habari kubwa ni kwamba usipolipia unaweza kufurahia chanel 5 muhimu  za nyumbani bure kabisa!!
 STARTIMES ENJOY ULIMWENGU WA DIGITAL WA TANZANIA

.
.
Next Post Previous Post
Bukobawadau