SOKA (MPIRA WA MIGUU)HUKO KASHARUNGA MULEBA
Diwani Kata ya Kasharunga wilayani Muleba Alhaji Khalid Hussen akigawa zawadi kwa mshindi wa ligi ya Diwani,kama ilivyokuwa azma yake ambapo Kasharunga FC mshindi wa kwanza Kasharunga Fc wamepata Tsh.100,000/-
na mpira,Mshindi wa pili Runazi kupata 75,000/-Mshindi wa tatu Nyakachuro FC walipata Tsh 50,000 na kila
timu shiriki ilipewa Tsh.15 000/-na mpira wa miguu mmoja ambapo gharama ya uendeshaji na vifaa vya michezo
kwa timu nane zilizoshiriki vilifikia thamani ya Tsh 2.5mil.
Diwani Kata ya Kasharunga wilayani Muleba Alhaji Khalid Hussen akigawa vifaa vya michezo kwa timu zilizoshiriki ligi yake
Na Shaaban Ndyamukama
MULEBA: Ligi ya diwani kata ya Kasharunga wilayani Muleba Mkoani Kagera juzi imemalizika hatua ya kuchezwa fainali baada ya timu ya Kasharunga kuibuka kidedea dhidi ya Runazi Stars ya katani humo kwa kuichapa bao 1-0

Tangu kuanza kwa mchezo huo timu zote zilishambuliana kwa
nguvu lakini hakuna mchezaji aliyeweza kuwaona
walinda milango kutikisa vyavu za timu pinzani licha ya kuhudhuriwa na
umati mkubwa wa watu na kutangazwa kupitia vipaza sauti.
Katika fainali hiyo timu hizo zilicheza bila kufungana katika
dakika 90 na kwenye dakika 30 za nyongeza ndipo kasharunga walifunga kupitia
kwa Mudasiri Hemed ambapo licha ya goli
hili kuingia wachezaji wa timu ya Runazi hawakuridhika
Katika kuimarisha
mahusiano ya kimichezo diwani wa kata hiyo Alhaji Khalidi Hussen alishauri
mpira huo kuisha na kugawa zawadi kama ilivyokuwa azma yake ambapo Kasharunga FC kuipatia Tsh.100,000/-
na mpira Runazi kupata 75,000/-
Mshindi wa tatu Nyakachuro FC walipata Tsh 50,000 na kila
timu shiriki ilipewa Tsh.15 000/-na mpira wa miguu mmoja ambapo gharama ya uendeshaji na vifaa vya michezo
kwa timu nane zilizoshiriki vilifikia thamani ya Tsh 2.5mil.
Alhaji Khalidi Hussen kabla ya kukabidhi zawadi hizo alisema kuwa lengo la kuekwa kwa ligi hiyo ni kuwaweka vijana kuwa pamoja na kujenga mahusiano ya karibu ili hatimaye wajiunge pamoja kuanzisha miradi ya ujasiliamali

Alisema vijana wengi wanashindwa kujikomboa kimaisha na
kubaki tegemezi ana ombaomba kwa kile alichokiita kubweteka na kujadili maisha
ya wanasiasa na majukumu yao bila wao vijana kujiendeleza kwa kuwa na miradi ya
maendeleo
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili katika kata
hiyo wakiwemo makocha watimu mbalimbali
walisema mzunguko wa ligi ulikuwa ni wa kusisimua na kuwaweka watu katika hali
ya furaha burudani na na amani
Pamoja na hayo refa wa mchezo huo aliyetambulika kwa jina la
Maximilian Yusuph na kocha wa Runazi
stars Jackso Tibalibusha nao walidai licha ya mchezo huo kuwa na ubishi wakati
wa fainali bado unawajengea umoja.