Bukobawadau

TASWIRA KATIKA PICHA MAAFA YA MVUA KIJIJINI BULEMBO KAMACHUMU

 BUKOBA;Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali imesababisha familia zaidi ya 125 kupoteza makazi baada ya nyumba zao kubomolewa na mashamba kuharibiwa katika Kijiji cha Bulembo kilichopo kata ya Kamachumu wilaya ya Muleba mkoani Kagera.
Hali ya migomba na mititi kufuatia upepo mkali.
 Wakazi wa kijiji hicho wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi kwa njia ya simu akiwemo mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage alisema maafa ni makubwa na msaada zaidi unahitajika kwani familia nyingi zipo nje ya nyumba zao na mvua zinaendelea kunyesha.
“Hali sio nzuri na timu ya watalaam ipo eneo la tukio ili kufanya tathmini zaidi kuhusiana na kadhia hiyo” alisema Mwijage na kuongeza kuwa kijiji cha Bulembo ndicho ambacho kimeathirika zaidi na vijiji vingine ambavyo vimekumbwa na kadhia hiyo ni pamoja na Buyago na Mafumbo.
Mwijage alisema athari kubwa kwa vijiji hivi vingine na vile vya jirani ni kuharibiwa mashamba yao lakini nyumba hazikuathiriwa sana na pia shule ya msingi Lugongo madarasa matano yameezuliwa paa na misaada mbalimbali imeanza kwenda kwa wahanga wa maafa hayo ikiwa ni pamoja na mahema, vyakula na dawa.
“Pia vijana wa msalaba mwekundu wanajaribu kurejesha paa upya katika nyumba ambazo zimeezuliwa” alisema na kuongeza kuwa baadae atakuwa katika nafasi nzuri ya kuweza kujua kiwango cha hasara ambayo imepatikana na misaada zaidi inayohitajika.
Shule ya msingi Lugongo madarasa matano yakiwa yameezuliwa paa
 Jengo la shule ya msingi Lugongo
 Mkazi wa kijiji cha Bulembo, Richard Kichabeba alisema hivi sasa familia hizo ambazo zimeezuliwa paa nyumba zao zinaishi nje na mbaya zaidi nyumba zaidi zinazidi kuporomoka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
 “Nyuma ikiezuliwa paa mvua zinakuja zinaimalizia kwani zikinyeshewa madongo na matofali yanaporomoka” alisema na kuongeza kuwa masomo yamesitishwa katika shule ya msingi Lugongo na misaada ya wahisani wa msalaba mwekundu haikidhi mahitaji.
Alisema manakijiji huyo kuwa aamilia moja inapewa blanketi moja wakati wapo watu hadi 20 na hata mgawo wa chakula haujakaa sawa na kimsingi alisema maisha yamevurugika katika kijiji hicho na kila zao shambani limeangamizwa.
 “Hakuna muhogo wala mgomba, barafu na upepo vimevuruga kila kitu,”alisema mkazi huyo na kuongeza kuwa mbaya zaidi hata hizo paa zao hazionekani zimehamishwa naupepo.
 Hakika hali ni tete.
 Utayari kwa zoezi la uokoaji
 Picha zaidi tembelea ukurasa wetu wa facebook ,tafuta BUKOBAWADAU INTERTAINMENT MEDIA AU JIUNGE NASI 'BUKOBAWADAU GROUP  KUPITIA FACEBOOK.
Hali ni mbaya na kumeendelea kuwapo na mfululizo wa mvua kubwa Mkoani Kagera.
JUINGE NASI KUPITIA FACEBOOK PAGE YETU 'BUKOBAWADAU INTERTAINMENT MEDIA'KWA PICHA ZAIDI NA MATUKIO MENGINEYO.
Next Post Previous Post
Bukobawadau