MKOA WA KAGERA WAKAMILISHA MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA MWAKA 2014
Mkoa wa Kagera unaendelea
kukamilisha maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa
utakaofanyika Mei 2, 2014 katika Uwanja wa Kaitaba Manispaa ya Bukoba kuanzia
saa 1: 00 asubuhi na kuendelea.
RS-KAGERA@2014
Katika kuhakikisha kila shughuli
iliyopangwa siku ya uzinduzi inafanyika kama ambavyo imepangwa Katibu Tawala
Mkoa wa Kagera Bw. Nassor Mnambila ametembelea uwanja wa Kaitaba uliofanyiwa
marekebisho makubwa na kujionea Halaiki ya watoto iinavyoendelea na mazoezi
yake.
Katika kutembelea uwanja huo Bw. Mnambila, zilifanyika shughuli zote
zitakazofanyika siku hiyo ya uzinduzi hasa watoto wa halaiki kuimba na
kuonyesha vitendo kwa kuumba maneno mbalimbali na mfano wa Mwenge wa Uhuru ili
kuhakikisha muda unazingatiwa siku ya uzinduzi.
Aidha Bw. Mnambila alitoa taarifa fupi kwa
waandishi wa habari kuhusu maandalizi
yalipofikia hivi sasa kwa kusema kuwa maandalizi hayo mpaka yanaendelea vizuri na
yamegawanyika katika sehemu kuu nne ambazo ni Kama ifuatavyo.
Kwanza ni Marekebisho ya Uwanja
wa Kaitaba ambao umefanyiwa marekebisho makubwa ya ujenzi wa vyoo vipya viwili, kurudisha mfumo
wa maji, kuezeka majukwaa ya pembeni matatu na
kurekebisha viti vyake, Kupakaa rangi na kuzungushia uzio mpya wa ndani,
kazi ambazo zipo katika hatua za mwisho kabisa.
Pili, Halaiki ya watoto, Bw.
Mnambila aliwajulisha Waandishi wa
Habari kuwa watoto wa Halaiki kwa hivi sasa wameishaiva kupitia walimu wao na
kinachosubiriwa ni siku yenyewe ya
uzinduzi aidha bado wanaendelea kufanya mazoezi ili kujiimarisha vizuri zaidi.
Tatu ni Wageni waalikwa ambapo alisema kuwa wageni wa Kimataifa,
Kitaifa na Mkoa tayari wamepelekewa mialiko ya kushiriki uzinduzi huo ili wahudhurie na
kushiriki na wananchi wa Mkoa wa Kagera siku ya tarehe 2/05/2014
Nne Bw. Mnambila aliwashukuru
Wadau, Watu binafsi, Taasisi mbalimbali, Wabunge na wananchi wote ambao waliombwa na kutoamichango
yao kuchangia uzinduzi huo wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru mwaka 2014.
Mwisho kabisa Katibu Tawala wa
Mkoa wa KageraBw. Mnambira aliwaomba wananchi wa mkoa wa Kagera kuhudhuria kwa
wingi siku ya Uzinduzi ili kushiriki pamoja katika tukio la kihistoria kwa Mkoa
wa wetu Kuzindua Mbioa za Mwenge wa
Uhuru Kitaifa
Imeandaliwa na:Sylvester Raphael
AFISA HABARIRS-KAGERA@2014