NGARA YAJIPANGA KUFAULISHA KWA KIWANGO KIKUBWA KATIKA BRN
Mwalimu mkuu shule ya
msingi Ntanga Mwl. Sendabaye Justus akikabidhiwa kinyago baada ya shule yake kupata ufaulu wa
wastani wa 16% matokeo ya darasa la saba mwaka jana
Katibu Tawala wilayani Ngara Ndugu Vedastus Tibaijuka akikabidhi kinyako kwa Mratibu elimu kata ya Murusagamba Ndugu George Rwetabura
Picha zote na habari kwa hisani ya ya Shaaban Nassibu Ndyamukama kutoka Ngara.
Mratibu elimu kata ya Murusagamba Ndugu George Rwetabura akipokea kinyago kutoka kwa katibu Tawala wilayani Ngara Vedastus Tibaijuka baada ya kata yake na tarafa kupata ufaulu duni wa 39% kwa kata & 52% kwa tarafa
Katibu Tawala wilayani Ngara Ndugu Vedastus Tibaijuka akikabidhi kinyako kwa Mratibu elimu kata ya Murusagamba Ndugu George Rwetabura
Picha zote na habari kwa hisani ya ya Shaaban Nassibu Ndyamukama kutoka Ngara.
Mratibu elimu kata ya Murusagamba Ndugu George Rwetabura akipokea kinyago kutoka kwa katibu Tawala wilayani Ngara Vedastus Tibaijuka baada ya kata yake na tarafa kupata ufaulu duni wa 39% kwa kata & 52% kwa tarafa
Pichani ni Mwalimu mkuu shule ya
msingi Ntanga Mwl. Sendabaye Justus
IDARA ya
elimu ya Msingi wilayani Ngara Mkoani Kagera
imejiwekea mikakati ya kukutekeleza
malengo ya kitaifa ya Big Results Now kwa 70% baada ya kupata walimu wapya
139 mwaka huu watakaoungana na 1543
waliokuwepo awali.
Katika
utekelezaji huo wazazi , walimu na wanafunzi
katika shule , na kata zilizoko tarafa ya Murusagamba wilayani humo wametakiwa kuongeza juhudi za kuinua
kiwango cha taaluma katika tarafa hiyo
ili kuingia katika wa malengo hayo
Ofisa elimu
idara ya msingi wilayani Ngara Simon Mumbee alisema hayo juzi kwenye maadhimisho ya wiki ya elimu wilayani humo na
kudai tarafa hiyo iko nyuma kitaaluma
katika shule zake 13 zilizoko kata ya
Muganza na Mursagamba
Mumbee
alisema tarafa hiyo imekuwa ya mwisho katika ufaulu wa mitihani ya darasa la
saba mwaka jana kwa kupata 52% ya wastani wa ushindi kitaifa ambao ni 60% na
kata ya murusagamba ilikuwa ya mwisho kiwilaya kwa ufaulu wa 39%
Alisema kuwa
katika wastani wa ufaulu kitaifa mwaka jana wa 60% tarafa ya Kanazi ilifaulisha
kwa wastani wa 76%,Rulenge 71% na Nyamiaga 70% na kwamba wilaya hiyo ilikuwa na
wategemewa wa kufanya mtihani 3913 katika shule 118.
Alifafanua
kuwa mwaka jana wilaya hiyo ilikuwa na watahiniwa waliofanya mtihani walikuwa 3861 wavulana 1790 na wasichana 2071 sawana 99%
ambao walifaulu ni 2683 wavulana 1311
wasichana 1372 sawa na wastani wa 69.5%.
Aidha
aliongeza kuwa pamoja na ufaulu huo bado katika shule 903 zilizoko Mkoani
Kagera shule ya msingi Ntanga kata ya
Murusagamba wilayani humo ilikuwa ya mwisho
kimkoa kwa kuwa na wastani wa 16%
“Napenda
kuwatia moyo uongozi wa tarafa kata na shule wakiwemo wazai na wanafunzi
wenyewe kuoneza juhudi ili kuweza kufanya vizuri kwa matokeo ya mitihani mwaka
huu”Alisema Mumbee
Aliongeza kuwa
idara ya msingi wilayani humo ina jumla
ya shule za msingi 118 kati ya hizo shule nne ni za binafsi na nyingine za serikali zote zinao wanafunzi wa elimu ya awali 12188 kati yao
wavulana ni 5292 na wasichana ni 5356.
Pia shule hizo zinawanafunzi wa darasa la kwanza
hadi la saba wapatao 73978 kati yao 36758 ni wavulana na 37220 ni
wasichana ambapo wanafunzi wa elimu ya MEMKWA ni 2200 kati yao wavulana
ni 1355 na wasichana 845.
Kwa upande
wake afisa elimu Taaluma Fidelis Apolinari
alizitaja shule zilizofanya vizuri katika
mtihani na kutuzwa zawadi na
vyeti vya taaluma bora kuwa ni Prince (English Medium) ya kwanza kiwilaya,
kimkoa na ilikuwa ya saba kitaifa
Alitaja pia
shule ya Mwanga (English Medium) ambayo ilikuwa ya pili kiwilaya ya tano kimkoa na 14 Kitaifa huku Rhec (English Medium) ilikuwa ya tatu kiwilaya na saba kimkoa ambapo kitaifa ni ya 17 kati ya shule
Alisema shule
nyingine ambazo ni shule za serikali zilizofanya vema ni Murgwanza Ngara mjini , Murukukumbo,
Kabalenzi , Mubinyange, Nakatunga na Ntungamo ambapo kata ya kwanza ni Ngara
mjini yenye ufaulu wa wastani (98%)
“Shule zenye
taaluma hafifu ni Ntanga ,Murugunga ,Rusengo Kabaheshi
Kirushya,
Nyankende ,Ntobeye, Kasulo, Kanyinya na Kabulanzwili”. Alisema
Kwenye
kilele cha wiki ya elimu iliyopambwa kwa kauli mbiu isemayo Elimu bora
Kuboresha Mtanzania katika wilaya hiyo kata tarafa na shule ilizokuwa za mwisho
zilizawadiwa vinyago na cheti chenye taaluma hafifu.
Pamoja na
taarifa hiyo Katibu Tawala Vedastus Tibaijuka kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya
Ngara Costantine Kanyasu katika hotuba yake aliwataka walimu kufanya kazi kwa
uadilifu ikiwa ni pamoja na kuboreshewa mazingira ya kufundishia
Tibaijuka
alidai walimu katika wilaya hiyo
wanahitaji kuwa na nyumba za kuishi katika shule zao kupata zana bora za
kufundishia na kupata mafunzo elekezi katika kuwaongezea ujuzi na maarifa
kulingana na mabadiliko ya teknolojia.
Alitaja
baadhi ya changamoto katika utoaji wa taaluma kuwa ni ulevi wa walimu na
kujihusisha na biashara ya bodaboda saa za kazi , mikopo mingi katika taasisi
za kifedha na hatimaye kushindwa kuwajibika kiutumishi na kifamilia.
MWISHO.