TAFADHALI PITIA HABARI HII MSAADA WAKO WA HALI NA MALI UNAHITAJIKA KWA DADA YETU!
Ndugu Msomaji wetu Ukiguswa na Habari hii tafadhali
toa chochote kwa Binti huyu pichani hakika anahitaji msaada wako.Binti huyu anajulikana kwa
jina la Phidea Furgence miaka 24 alijifungua watoto 3 wa kike wenye umri wa miezi 3 kwasasa.
Mungu akubariki, tuwahurumie watoto hawa Malaika wa Bwana!!
Phidea anomba msaada wa kuwalea
watoto wake ili wapate kukua kwani anasema watoto hao hawezi kuwanyonyesha
maziwa ya mama tu yakawatosha wote watatu mpaka kukua. Binti huyu ameolewa na
Dionizi John mwendesha bodaboda.
Pamoja na mmewe kumjali lakini
anasema kipato hakitoshi kwani anahitaji pia msaidizi wa kuwalea watoto hao na
kuwapatia lishe bora ndiyo maana aliamua kutembelea ofisi mbalimbali kuomba
msaada.
Aidha Phidea anaishi Mtaa wa
Nyangoye Manispaa ya Bukoba na mara ya Kwanza alijifungua watoto mapacha wawili
wa kiume kwa sasa wana umri wa miaka 4
kwahiyo Phidea ana watoto 5 kwa sasa.Unaombwa msaada wako wa hali na
mali kama fedha na mahitaji mbalimbali kama chakula kwa wtoto hawa. KumbukA
Phidea hana mgogoro wowote na mmewe pia wanashirikiana vizuri ila uwezo wa
kuwamudu watoto hawa wa kike watatu kwa pamoja ni vigumu ndo maana anakuomba
msaada wako.
Unaweza kuwasiliana na Binti huyu
kwa njia ya simu namba yake ni 0752 922 937 kama una la kumsaidia. Kumbuka
binti huyu ana kazi kubwa ya kuwalea watoto wake itakuwa si busara kutumia
nambayake kwa kumsumbua au kuongea mambo ambayo hayapaswi kwani ni fundi
cherehani lakini ameacha kazi yake kuwalea watoto hawa.Mungu akubariki, tuwahurumie watoto hawa Malaika wa Bwana!!