TANZIA: KIFO CHA TA PAULO KILAINI ( BABA YAKE ASKOFU METHOD KILAINI)
Habari
tulizozipokea asubuhi ya leo Alhamisi Aprili 3,2o14 na kuthibitishwa na mtu wa karibu ya familia ya Baba Askofu Method Kilaini ya kuwa
Baba yake mzazi ,Ta Paulo Kilaini amefariki dunia mapema ya leo huko Jijini Dar es salaam.
Taarifa za awali zinasema mwili wa Marehemu utasafirishwa siku ya Jumamosi ,na shughuli za mazishi kufanyika siku ya Jumatatu Aprili 7,2014 saa 8 mchana Kijijini Katoma Bukoba.
Tutaenelea kutoa taarifa kadri tutakapokuwa tunapata habari kuhusiana na msiba huu.
BUKOBAWADAU BLOG tunatoa pole kwa Ndugu na jamaa wa familia,Pole Baba Askofu Kilaini, Mwenyezi Mungu Raha ya milele ampe Marehemu Ta Paulo Kilaini, na Mwanga wa milele amwangazie.!!!