UBELGIJI WATEKETEZA TANI 1.5 ZA MENO YA TEMBO
Picha inaonesha meno ya tembo na Mtambo wa kuteketeza meno hayo. Leo hii
Serikali ya Ubelgiji imeteketeza meno ya tembo tani 1.5 iliyoyakamata
yakiingingizwa Ubelgiji. Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus
Buberwa Kamala ameipongeza Serikali ya Ubelgiji kwa hatua hiyo na
ameziomba nchi nyingine zenye soko la meno hayo kuchukua hatua kama
ilivyofanya Serikali ya Ubelgiji. Aidha, Balozi Kamala ameziomba nchi
zilizoendelea kusaidiana na nchi zinazoendelea kupambana na ujangiri.