WAISLAMU MULEBA WAZUIWA KUFANYA MIHADHARA
Shekhe wa wilaya ya Muleba Zacharia Kagimbo
MULEBA: WAUMINI wa dini ya kiislamu katika
mji wa Muleba Mkoani Kagera juzi wamezuiwa na jeshi la polisi wilayani humo kuendelea
na mhadhara wa dini yao kwa madai kuwa ulilenga kukashifu dini ya Kikristu
Wakiongea naMwanahabari hizi katika mji huo nchi waumini hao walisema kuwa
mhadhara huo wa siku tatu katika mji wa Muleba uliendeshwa na wahadhili kutoka
jijini Dar es Salaam wakilenga kubainisha ukweli baina ya Uislamu
na Ukristo.
Imamu wa
msikiti wa ijumaa wa Masjidi Nuru aliyejitambulisha
kwa jina la Issa bin Sued katika mji huo alisema kuwa mtafaruku huo ulichangiwa
na kiongozi wa BAKWATA wilaya ya Muleba
Sheikh Zacharia Kagimbo kutopenda
mhadhara huo
Alisema
katika kutoa mhadhara huo wahadhiri walifafanulia waislamu kuwa katika uislamu
mwenyezi Mungu alikuwa na manabii wengi kabla na baada ya kuwepo mtume Mohamadi saw na
kwamba miongoni mwao ni nabii Issa mwana wa Mariam
Alidai mara
baada ya waislamu kuhudhuria na baadhi
ya wasikilizaji wa imani ya kikristo walianza kulalamikia mhadhara huo kwa kusikia kuwa nabii Issa sio Mungu wala mtoto
wa Mungu kama wasemavyo waumini wa dini nyingine
Aidha
alisema kuhusiana na hali hiyo wakristo walilalamika hata kwa mbunge wa jimbo
la Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka
na mkuu wa wilaya kisha kumfuata
shekhe wa wilaya ya Muleba Zacharia kagimbo
na kulalamikia hilo
“Wahadhili
walikuwa na vibali kwani walishazunguka nchi nzima kwa mkoa wa Kagera walisha
pita wilaya nyingi hivyo kuzuiliwa ni kuwakosesha haki kupata elimu ya dini
yao”.Alisema Imamu Issa Sued.
Aliongeza
kusema kuwa wakati mhadhara wa dini ukiendelea waliona jeshi la polisi
likiwafikia wahadhiri hao na kuwataka wafunge vilago kuondoka kwani mahubiri yao yanalenga kuhatarisha
usalama wa kiimani baina ya dini mbili
Kwa
upande Hilali dini Kipozeo
ambaye ni mmoja wa wahadhiri na makamu mwenyekiti wa Mihadhara kanda ya ziwa katika kulingania
waislamu alisema hawakuwa na nia ya kukashifu dini nyingine bali wanaeneza dini
yao.
Alisema kuwa
jeshi la polisi lilifika kwa shinikizo la viongozi wa serikali na kiongozi wa
BAKWATA wilayani Muleba na kwamba hakuna mhadhiri aliyeumizwa wala kuamatwa na
malengo yao ni kueneza dini kupata waumini wengi wa kiislamu
“Mtume
Mohamad SAW alipata mitihani wakati akieneza dini ambapo aling’olewa na
meno hili sio geni kwetu kwani ulimwengu huu vita kubwa ni
kuangamiza uislamu”.Alisema Kipozeo
Alisema kuwa
safari ya wahadhiri hao imelenga kwa mikoa ya kanda ya ziwa ambapo kwa mkoa wa
kagera walishatembelea wilaya ya Biharamulo Karagwe Muleba Bukoba manispaa
Misenyi hadi Kampala nchini Uganda.
Hata hivyo Kiongzo
wa BAKWATA wilayani Shekhe Zacharia
Kagimbo amekanusha kutohusika na vurugu hizo na kwamba hakuwa na taarifa za
kuwepo kwa wahadhiri hao kueneza dini yao na kusambaza ujumbe wa Allah SW.
Alisema
taarifa za kuwepo vurugu za mhadhara
alizipokea kutoka jeshi la polisi ngazi ya wilaya hasa kwa OCD na kwamba hakuna
kiongozi wa mtaa wa Muleba mjini wala msikiti wa Nuru aliye mtaarifu kuwepo kwa
wageni hao
Alishauri
kwa wale wanaohitaji kueneza dini ya kiislamu wilayani humo kuzingatia taratibu
kwa kuwaona viongozi wanaohusika na maeneo ikiwa ni pamoja na kupitia kwenye
vyombo vya usalama ili kulinda amani na utulivu kwa dini zote.
Na shaaban
Nassibu.