BALOZI KAMALA AWEKA SAHIHI HATI YA MAPOKEZI YA HAINAUT
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiweka sahihi Hati ya Mapokezi ya Hainaut huku Gavana wa Hainaut Mhe. Tommy Luclercq akishuhudia. Mhe. Luclercq alimshukuru Balozi Kamala kwa kuandaa ziara ya wadau wa reli na bandari kutoka Tanzania waliotembelea Ubelgiji na alibainisha kwamba angependa kuona ushirikiano wa Tanzania na Ubelgiji ukiimarika siku hadi siku.